Wengfine wanasubiri kama wapiganaji wa msituni sijui yakitolewa matokeo mapya itakuwaje?
Viongozi wa Chadema wanabidi waongezewe ulinza kwani hali inaonekana kuw ambaya zaidi wakiambiwa kuwa wamesababisha kifo.
Panoja na kuwapo kwa polisi lakini vijana wanaleta vurugu nyingi kiasi kwamba tumepata taarifa kuwa kuna wengine wanaletwa kw amagari nadhani sasa siasa inakolea msibani!!!!!
Wangwe ahofiwa kupigwa risasi
Zengwe limekolea kijijini kwa Chacha na ndugu wamegoma mwili wa ndugu yao kuzikwa ili kuruhusu uchunguzi zaidi wa kifo chake ufanyike kutokana na hisia za wanafamilia kwamba, alipigwa risasi
Kaka wa marehemu, Prof Samuel Wangwe alisema kuwa, kutokana na kifo hicho kuwa na mashaka mengi, familia imeamua kufanya uchunguzi wa kina ili ijiridhishe na sababu za kifo cha mbunge huyo.
Akizungumza katika hadhira iliyokusanyika nyumbani kwa marehemu kijijini Kemakorere, Prof Wangwe alisema kuwa, familia imepata mashaka makubwa kutokana na mambo mengi na hasa sababu za kifo ambazo zimedaiwa kuwa ni ajali.
“Mambo mengi yamesemwa, sisi kama familia tumeamua kufanya uchunguzi huru na wa kina ili kubaini sababu ya kifo cha marehemu, katika uchunguzi huu familia itatoa daktari wake na serikali,” alieleza.
Alisema kuwa familia imeamua kusitisha maziko hayo kutokana na mwili wa marehemu kubainika kuwa na jeraha ambalo wanadhani limetokana na kitu kingine na wala si ajali ya gari kama ilivyoelezwa.
Alipoulizwa na gazeti hili iwapo familia imefanya uchunguzi wa awali na kubainika kuwa kifo cha marehemu kimetokana na kushambuliwa kwa risasi, Prof Wangwe alisema kuwa ni kutokana na utata huo familia imeamua kufanya uchunguzi wa kina kwa kuzingatia taratibu na sheria.
“Ni kweli mwili wa marehemu umekutwa na jeraha, lakini mimi sijaliona; na wala sijui kama ni la risasi, lakini kikubwa tunafanya uchunguzi kesho (leo) ili kuondoa utata wote huo, hii ni haki ya familia tumetaka hivyo na serikali imeridhia,” alieleza.
Kwa upande wa serikali, msemaji wa serikali, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira, alisema kuwa serikali imeridhia kufanyika kwa uchunguzi huo ambapo familia itatoa wataalamu wa kufanya uchunguzi na serikali kutoa mwakilishi wake.
“Serikali imeruhusu uchunguzi huru ufanyike ambapo utahusisha daktari wao wa familia na sisi kwa upande wetu serikali tutatoa daktari pia,” alisema Wasira.
Habari ambazo timu ya waandishi wetu walioko Tarime na Kijijini kwa Wangwe walizopata kutoka ndani ya familia, zilisema kuwa uchunguzi wa mwili huo ulifanywa na Dk Turwa Mrimi, ambaye alibainisha kuwa mwili wa marehemu ulikuwa ukionyesha kuwa alipigwa risasi mdomoni na kutokea nyuma ya shingo, pamoja na kuwa na jeraha lililoonyesha kuchomwa na kitu chenye ncha kali pajani kulia.
Kutokana na hali hiyo, ndugu walilazimika kukaa kikao na kujadiliana hatima ya hali hiyo, huku wakifanya mawasiliano kuagiza daktari mwingine zaidi.

No comments:
Post a Comment