Tuesday, September 30, 2008

FIRST CHILDREN

Vitegemezi vya JK Rashid (kulia) Kikwete , Mohamed na Khalfan Kikwete wakiwa wamejumuika na watoto wa vituo vya kulelea watoto yatima jijini Dar es Salaam juzi katika futari ya pamoja ambayo aliwaandalia Ikulu

5 comments:

Anonymous said...

kwa hiyo kuna first lady na first children?!~
Hii ya vitegemezi vya JK sijafahamu maana yake, hebu wadau ni elimisheni.

Anonymous said...

Kwa kifupi maana yake watoto wa JK

Anonymous said...

Hawa watoto wanaonekana ni wakorofi sana!!!

Mswahilina said...

Ahaa, mzee wa Sumo; inaonekana siku hizi huna cha kutuonyesha.

Au unataka hawa watoto wa Mkuu wa Nchi waendelee kuonekana kwa mwezi mzima ili upewe "Ukuu wa Wilaya" kama rafiki yako Michuzi?

Haya we, hii nayo ni mbinu ya kujulikana.

Anonymous said...

Watu kwa roho mbaya hata watoto mnawasema vibaya! Wewe unayesema watoto wa mwenzio wanaonekana wakorofi, huo ukorofi wao umeuona wapi? Wameufanya wapi? Hebu jamani hawa ni malaika wadogo hawajui hata kinachoendelea nini zaidi ya kujiona wanakaa jumba kubwa basi! Wivu mwingine bwana hauna hata maana! Halafu kuna ajabu gani watoto wa Rais picha zao kuonekana? Mbona ni kitu cha kawaida ulimwenguni, watu walimwona Chelsea Clinton tangu yuko mdogo mpaka leo anaonekana akiwa mama mzima, kubali kataa mtoto wa Rais si mwenzio tena keshakuwa selebriti wajisemea wazungu!