Tuesday, September 16, 2008

WALIMU WA BONGO

Mkurugenzi K'ndoni awatosa walimu 200



Wakatembea kutoka kwa Mkuu wa mkoa hadi Manispaa ya kinondoni, Mkurugenzi nae akawatolea nje.
Walisubiri majibu, ikawa hola, lakini baadae Afisa alimu alisem akuwa anawatambua kuwa walimu wa shule za msingi na alishawapangia vituo vya kazi.
Wakasubiri weee baadae wakachoka kwani hakuna kilichoeleweka! Walimu jamani mimi naona wanastahiri kuheshimiwa ndio waliotufanya kujione wajanja mjini sasa hivi! ama uongo jamani hii ni nnoma.

MKURUGENZI wa Manispaa ya Kinondoni amewakana zaidi ya walimu 200 waliondamana hadi ofisini kwake kudai fedha za kujikimu ambazo hawajapewa tangu waripoti katika vituo vyao vya kazi mwezi Mei mwaka huu.

Akizungumza baada ya kupokea maandamano hayo, mkurugenzi wa manispaa hiyo, Noel Mahyenga alisema, hahusiki na walimu hao na wala hawatambui kama waajiriwa wa manispaa yake.

"Wanatakiwa kurudi ngazi ya mkoa ili kuangalia sehemu watakapowaweka kwa kuwa manispaa yangu haina upungufu wa walimu, ingawa tatizo hili nalifahamu," alisema mkurugenzi huyo.

Alipotakiwa kutoa maelezo kuhusu mshahara waliolipwa mwezi walioanza kufanya kazi, mkurugenzi huyo alidai kuwa, walilipwa kimakosa na kwamba kama watabahatika kupata sehemu za kwenda, ataongea na wizara ili wakatwe mshahara huo.

Akizungumzia suala hilo, Afisaelimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Makali Bernard alikiri kutokea tatizo hilo na kuongeza kuwa hahusiki.

"Nilishamaliza kazi ya kuwapangia vituo vya kufanyia kazi. Nashangaa kusikia kwamba Manispaa haiwatambui kama watumishi wao," alisema. "Kazi yangu ni kugawa vituo kama ninavyoagizwa na wizara. Hilo ni suala la mkurugenzi wa manispaa ambaye ndiye mwajiri wao."


No comments: