Monday, September 22, 2008

YANGA INATISHA
MABINGWA wa soka Tanzania, Yanga ya Dar es Salaam imeendeleza wimbi lake la ushindi baada ya kuitandika Villa Squad ya Kinondoni mabao 5-0 katika mchezo usiokuwa wa ushindani kwenye Uwanja wa taifa, Dar es Salaam.
Yanga ambayo sasa imefikisha pointi 15 kutokana na kushinda mechi zake zote tano, ilifunga mabao matatu ndani ya dakika nane, bao la kwanza katika dakika ya 14 wakati bao la tatu dakika ya 21.
Hata hivyo, shujaa wa mchezo huo kwa Yanga ni Boniface Ambani ambaye peke yake alifunga mabao matatu katika mchezo huo na kufikisha idadi ya mabao nane

No comments: