Monday, October 13, 2008

CHADEMA YASHINDA UCHAGUZI TARIME






Ni kwamba tumepigwa mabomu ya kutosha hapa mjini kwajana na leo siandiki kepsheni kama mtu amekasirika asisome tena hii blog!

7 comments:

Anonymous said...

poleni sana ila nimefurahi kusikia ushindi huu, ni muhimu nchi yetu ipate nguvu ya upinzani. Nchi zilizoendelea upinzani una nguvu mfano Amerika na uingereza. Kuhusu kushinda kiti cha uraisi wanahitaji programme za muda mrefu kwa kuwa bado kuna sehemu ccm siyo ya kuondoka leo ama siku za karibuni(2010). Hongera chadema.

Anonymous said...

Mbona hizi picha zinajitosheleza bila captions

Anonymous said...

pole sana mzee wa sumo na ahsante kwa kutuletea habari hizi kwa picha zinazojitosheleza bila hata ya caption. watanzania tuamke saa yakuiondoa ccm ni sasa

Anonymous said...

kwani pole pole ndio mwendo,na dalili ya mnvua ni mawingu...2010 sio mbali tumechoka kwa kununuliwa na doti za khanga na pishi moja ya mchele.na kuwapigia klura wanaondeleza ufisadi,bot,epa,n.k ..watanzania tumeshaamka sio mafala tena..kama mzee makamba na kauli yako eti mtoto wa dereva atabakia kuwa dereva..basi alama ndio hiyo sisi watoto wa madereva na wakulima kamwe hutapata kura zetu ..hata mkitumia hell-copter au hell-chopper 500 za kukodi hamtupati ng'ooooo salamu ndio hizo

Anonymous said...

Wapinzani wajaribu kuwaelimisha wananchi au wanachama wake kwamba watu wote Tanzania ni sawa ila tofauti ya vyama vya upinzani ni agenda na tuache siasa za kupigana na kuuwana.Tanzania inabidi tutoe mfano kwa Afrika nzima.Tuelimishe wanachama wa ccm na vyama vya upinzani ya kwamba wote ni watanzania na tofauti ni agenda. Pili, vyombo vya dola vinatakiwa kutochagua upande. Nilazima sasa serikali zetu ziwe makini na vyombo vya dola na kuweka sheria zitakazo wazuia vyombo vya dola kupiga wananchi na kuzuia watu kufanya maandamano ya amani.....mwisho wananchi ndiyo wataitoa ccm madarakani na watu lazima wajiandikishe kupiga kura....

Anonymous said...

Mtanzania apata ajali Marekani, agongwa na mtoto aliyeiba gari!



Kijana wa Kitanzania Bw. Ndalima Nzaro yuko mahututi kwenye hospitali ya Chuo Kikuu cha Michigan, Ann Arbor, nje kidogo ya Jiji la Detroit nchini Marekani baada ya ajali iliyosababishwa na kijana wa miaka 15 aliyeiba gari kugonga gari la Ndalima lililokuwa limesimama kwenye taa za kuongozea magari likisubiri rangi ya kijani.

Kijana huyo aliyegonga gari alikuwa anafukuzwa na Polisi. Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa mji mdogo wa Westland kijana huyo aliyeiba gari na ambaye hakuwa na leseni ya kuendesha gari alikuwa anaendesha kwa kasi zaidi ya maili 100 kwa saa na aliyagonga magari ubavuni yaliyokuwa yamesimama hapo kwenye taa za kuongozea magari kwenye barabara ya Merriman.

"Wale madereva waliokuwa wanasubiri rangi ya kijani kuwaruhusu hawakuwa na jinsi yoyote ya kukwepa ajali hiyo" alisema Chifu Jim Ridener. Bw. Ndalima aliyekuwa anaendesha gari ndogo aina ya Honda Accord, alitibiwa kwa dharura kwenye hospitali ya Garden City lakini kutokana na majeraha yake aliitiwa Helikopta ya Hospitali ambayo ilimchukua na kumkimbiza kwenye hospitali ya Chuo Kikuu cha Michigan mjini Ann Arbor.

Hospitali hiyo ni mojawapo ya hospitali zenye uzoefu mkubwa katika kuhudumia dharura za ajali katika eneo hili la Michigan. Mtoto huyo wa miaka 15 alikuwa anaendesha gari aina ya Mercedes Benz S55MG ambalo ni la rafiki ya kiume wa mama yake. Kutokana na kijana huyo kuwa chini ya umri jina lake halitajwi kwenye vyombo vya habari.

Hata hivyo kijana huyo yuko mikononi mwa Polisi wakati uchunguzi ukiendelea na mashtaka dhidi yake yatategemea hali ya Ndalima inaendeleaje.Habari ambazo tunazipata sasa hivi, hali ya mgonjwa siyo nzuri.Tutawaletea habari zaidi kwa kadiri tunavyozipata.

Agepe said...

Wow... nice blog. Nice picture. Tx for your post. Greetings....