Saturday, October 04, 2008

HAYA NDIO MAMBO YENU?


Familia moja ilishangazwa pale walipopokea jeneza la marehemu mama yao aliyefariki nchini Marekani. Lilitumwa na mmoja ya watoto wake wa kike.

Mwili ndani ya jeneza ulikuwa umesongwa sana ndani ya jeneza kiasi kwamba uso wa marehemu ulikuwa umegusa kioo cha jeneza! Walipofungua jeneza, walikuta barua juu ya merehemu, iliyosomeka namna hii:
'Wapendwa ndugu zangu, nimeutuma mwili wa mama yetu kwa ajili ya mazishi, kwani imekuwa siku zote hamu yake kubwa kuzikwa nyumbani Ileje, katika nyumba ya ukoo.
Samahani sikuweza kuja na mwili kwani nimenyimwa likizo kwani kuna upungufu wa wafanyakazi hapa kazini mwezi huu. Ndani ya jeneza, chini ya mwili wa mama, kuna makopo 12 ya samaki wa makopo, paketi 10 za supu ya Royco na chupa 8 za jam ya maembe.
Mgawane hivi kwa jinsi mtakavyoamua nyinyi. Katika miguu ya mama kuna pea moja ya viatu vya Reebok namba 9 kwa ajili ya mtoto mkubwa wa Mwakajinga. Pia, kuna pea mbili za viatu kwa ajili ya watoto wa Mwakipesile na Ipiana , natumaini nitakuwa sijakosea namba za miguu. Nimemvalisha pia mama American T-shirts 6, kubwa kabisa ni kwa ajili ya Mwakibibi, na zinazobaki ni za watoto wake.
Hizo jeans mpya 2 ambazo mama amezivaa ni za wavulana Mwakatumbula na Mwakitobe. Hiyo Swiss watch mkono wake wa kushoto ni zawadi ya Rhoida kwa ajili ya sikukuu yake ya kutimiza miaka 21. Anti Queen, hizo heleni, mkufu na pete ambazo mama amevaa ni zako.
Hizo soksi 6 ambazo mama amevaa wagaiwe wajomba. Tafadhali mgawane kama nilivyosema na kama kuna kitu kingine mnahitaji, basi mnieleze kwani hali ya baba nayo siku hizi si nzuri sana .
Dada yenu mpenzi, Mama Mpoki

8 comments:

Anonymous said...

Is this a true story ? Unbelievable !! Please say No!!

Anonymous said...

fun ad jokes mate

Anonymous said...

kwakweli huu si ukweli, inawezekanaje mtu akamfanyia mama yake wa kumzaa mambo hayo, ina maana uyo dada hana uchungu na mama yake. du mi siamini kabisa apo

Anonymous said...

we blogger administrater,MUOGOPE mungu

noor shija said...

kumamayo mpoki, kama ni kweli tuonyeshe picha.

by Noor Shija
e-mail nshija2002@yahoo.com

blogs: http://dagshija.blogspot.com/ or http://shija.blog.co.in/

Anonymous said...

Du! kweli duniani imeisha na kama sikuisha ni laana tupu na kama sio laana basi atakuwa anakwepa gharama jamani mimi siamini kabisa labda atoe picha du!

UTAMU said...

UTAMU Tumerudi upya tembelea http://theutamus.blogspot.com

Tafadhali mfahamishe na mwenzio... UTAMU KIBOKO WA MAFISADI WA NGONO

Anonymous said...

UNE NGANILE KANGI NGUKOMA NA PA NYUMA!! NTUNGULU UJO; ASYAGILE KUGU INONGWA ISI?