Thursday, October 30, 2008

WASTAAFU EAC WAZUA JAMBO!

Baada ya kuingia mtaaani wazee hao walionja mabomu ya mchozi.
Gari la Polisi wa FFUlikiwanyunyizia dawa ya macho na mapafu wazee hao.
Mkuu wa Mkoa, Abbas Kandoro, akiweka mkakati wa kuwafanyizia wazee hao na Kamanda wa Kanda ya dar es Salaam, Suleyman Kova.

Mmoja wa wazee hao akomwaga radhi!
Walianza wakiwa tuli barabarani hawakujua ambacho kingefuatia.

VIONGOZI wa serikali, wafanyabiashara wakubwa, mabalozi na wananchi wa kawaida jana walionjeshwa ukubwa wa machungu wanayopata wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wakati wazee hao walipoweka kizuizi katika eneo la daraja la Sarenda na kusababisha magari kushindwa kuingia katikati ya jiji.
Eneo hilo, lililoko makutano ya Barabara ya Ali Hassan Mwinyi na Umoja wa Mataifa, ambako kuna kituo cha polisi cha Sarenda, ndio njia kuu na pekee ya magari yote kutoka maeneo ya Oysterbay, Mikocheni, Msasani na Ada, ambako wanaishi viongozi na watendaji wakuu wa serikali, mabalozi na maofisa wengine wa taasisi za kimataifa hupitia.
Maeneo ya Kinondoni, Mwenge, Kawe, Tegeta na Mbezi ambako wanaishi wananchi wa kipato cha chini na kati, pia waliathirika na mbinu hiyo ya wastaafu wa EAC kuishinikiza serikali kuwalipa mafao yao baada ya jumuiya hiyo kuvunjika mwaka 1977.
Na kutokana na maeneo hayo kuishi vigogo wengi, msururu uliozuiwa ulikithiri 'foleni' za kawaida na kusababisha watu wengi kuchelewa makazini.
Wastaafu hao wanaokaribia 200 wanataka serikali iwalipe madai yao ya fedha ambazo wanadai, ambazo ni jumla ya Sh300 bilioni.
Katika kikao chao cha juzi kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, wastaafu hao walidai kuwa wangeamkia ubalozi wa Uingereza ambako walidai wangepiga kambi hadi suala lao litakapopatiwa ufumbuzi.
Lakini kiongozi wao, Nathaniel Mlaki akaeleza kuwa kabla ya kwenda ubalozini, wangepitia sehemu moja, ambayo hakutaka kuitaja na kuwahimiza wenzake kuwahi asubuhi ya jana ili waelezwe sehemu hiyo na kuwataka wabebe chupa za maji.
Baada ya kufika katika eneo hilo saa 12:20, wastaafu walilala barabarani huku wakisema maneno mbalimbali ya kuilaumu serikali kabla ya kuvua nguo baadhi yao, alisema shuhuda mmoja aliyekuwa eneo hilo wakati wa tukio.
Kutokana na hali hiyo magari yote yanayotumia barabara hizo yalikwama kwa muda wa zaidi ya saa mbili na nusu kabla ya wastaafu hao kuondolewa kwa nguvu na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU).

3 comments:

Anonymous said...

Lakini jamani hawa wazee wetu wanacho kidai si nihaki yao?sasa kwanini kuwanyanyasa kiasi hichi?basi hata heshima hii serikali haina?kikwete muogope muungu usikirie hapo ulipo utakuwapo maisha yako hao wazee wanahitaji kubembelelezwa kuliko unavyo wabembeleza hao mafisadi wenzako
hiyo sio aibu yao ni aibu yako wewe hivi kweli una lala na kupataga usingizi?

Anonymous said...

poleni wazee wetu mungu yupo haya yote yataisha siku moja
sio haki hata kidogo!

Anonymous said...

JK naomba afanye juu chini awatatulie tatizo wazee hawa.Najua anawathamini sana wazee na sasa awatatulie matatizo yao.Mkapa alijitahidi kwa uwezo wake,kuwapiga Tanganyika jeki ni kuwakosea na kujichumia laana bure za wazee hawa wasio na hatia kama MAFISADI WA EPA.