Friday, December 19, 2008

MGOMOJamani watu wananilaumu kwakuwa muda mrefu nilikuwa sikaupload blog hii, kwani hawajui kwamba kwa sasa nchi nzima watu walikuwa wamegoma? Mimi nikigoma kunakuwa na noma gani?
Tuache hilo nilikuwa kidogo kijijini kumalizia msiba wa Mzee Bukuku, hata hivyo watu tunahitaji kupumzika!
Lakini kinachonishangaza ni Mzee wangu hapo juu leo nadhania naweza kupata dhamana, lakini hizi tuhuma wanazompa kweli ameshindwa kuweka dhamana kama wakina Jeetu Patel ama Mzee Yona?
Isije ikawa nae hana kitu kama Mwakosya wa BoT mpaka ikabidi apate punguzo maalum? Tusikilizie leo. Nasikia wengine zaidi wanakuja!

No comments: