Friday, January 23, 2009

CHUO (UDSM) KIKUU MOTO

Viongozi wa wanafunzi wakiwa mahakamani juzi wakikabiliwa na shitaka la kuandamana na kubeba mabango.
Siku hiyo ndioyo walitiwa mbaloni wakiwa katika motokali ya polisi.

Hapa ndipo walipodakwa na sasa wamepata dhasmana ya sh 500,000 kwa mtumishi wa serikali na masharti ya dhamana ni pamoj ana kutofika eneo la chuo ama kuhusika katika maandamano mengine! Lakini sasa mambo yamebadilika hebu pata ya walimu wao wanasemaje?:

CHAMA cha Wahadhiri wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (Udasa) kimetoa tamko la kuutaka uongozi wa chuo hicho kuwarejesha wanafunzi wote waliosimamishwa ili waweze kuendelea na masomo yao kama kawaida.
Karibu theluthi mbili ya wanafunzi wa chuo hicho wamezuiwa kurejea chuoni kwa madai kuwa wameshindwa kutimiza masharti, yakiwemo ya kulipa sehemu za gharama za elimu baada ya chuo hicho kufungwa mwishoni mwa mwaka jana kutokana na wanafunzi kugomea sera ya uchangiaji elimu, wakidai kuwa inabagua.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, katibu mkuu na mjumbe wa Udasa, Profesa Josephat Rugemalira alisema kuwa utaratibu huo, ambao umewekwa na uongozi wa chuo, ni mbovu na ambao umesababisha usumbufu kwa wageni, majirani na wananchi wa eneo hilo kwa ujumla.
“Hivi sasa wanafunzi wameanza kurudi kwa makundi kama ilivyopangwa tangu Januari 19 mwaka huu, lakini kumekuwa na usimamizi usiokuwa wa kawaida katika maeneo haya, hali ambayo imeleta adha na usumbufu mkubwa kwa wananchi na wageni. Kutokana na hali hiyo, tumeutaka uongozi wa chuo kutekeleza tamko hilo kama tulivyolitoa,” alisema Profesa Rugemalira.
Aliongeza kuwa ili uweze kutatua matatizo yaliyojitokeza, uongozi wa chuo hicho ulipaswa kuangalia upya utaratibu mzuri wa udahili kwa wanafunzi hao ambao utasaidia kupunguza usumbufu chuoni hapo na kuangalia mustakabali mzima wa hadhi ya chuo hicho na taifa kwa ujumla.
Alisema utaratibu uliopo sasa wa kuwarudisha wanafunzi chuoni kwa kuwafanyia udahili upya baada ya kulipa ada zote za mwaka wa masomo 2008/09 kwa kufuata masharti yaliyowekwa na kuweka ulinzi mkali, sio mzuri na unasababisha usumbufu mkubwa.

No comments: