Saturday, February 14, 2009

KESI YA ZOMBE

Makelle aanza ushahidi, atupia mpira polisi wa Mlimani
WAKATI Ahmed Makelle, mshitakiwa wa tatu katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge mkoani Morogoro na dereva teksi wa Manzese jijini Dar es Salaam, akirusha mpira kwa askari polisi wa kituo cha Chuo Kikuu, mshtakiwa Christopher Bageni jana alikiri kuwepo kw autata katika vifo vya watu hao wanne.
Makelle, ambaye ni mrakibu msaidizi wa polisi, ASP, na pia ni shahidi wa tatu wa upande wa utetezi, alikuwa akitoa ushahidi wake jana akiongozwa na wakili wake, Majura Magafu katika kesi hiyo inayoendelea Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Lakini mvuto ulikuwa mwishoni mwa utetezi wa mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo, Bageni ambaye baada ya kubanwa na Jaji Salum Masati alikiri kuwepo kwa utata wa vifo vya watu hao wanne.
Jaji: Mshitakiwa,hebu kwanza nikuulize, hii ripoti ya daktari hapa mimi bado inanisumbua kidogo.Kwanza umesema ulipokwenda katika ukuta wa Posta ulipopelekwa na James hamkukuta damu
Bageni: Ni kweli
Jaji: Jana yake siku mliyokwenda ama asubuhi yake kulikuwa na mvua?
Bageni: Hapana
Jaji:Umesema ukutani uliona matundu sita yalidaiwa kuwa ni ya risasi, lakini hawa marehemu walikuwa ni wanne je hizi risasi sita zilitoka wapi au baada ya kupigwa waliendelea kupanda ukuta?
Bageni:Mtukufu Jaji.mimi sikuwepo lakini mapambano mengi zinaweza kupigwa risasi nyingi zikajeruhi chache tu.
Jaji:Na kwa nini hapakuwa na damu?
Bageni: Mtukufu Jaji,hata mimi sijui kuwa ilikuwaje.
Jaji:Umesema matundu yale jinsi yalivyokuwa ukutani inaonekana yalipigwa kutokea pembeni, je katika hali hiyo inawezekanaje kumpiga mtu kisogoni? Alihoji Jaji na kumuelekeza Bageni aegemee ukuta na kisha kumtaka eleze mtu akipiga risasi kutokea upande wa kushoto kwake ni jinsi gani inaweza kumpata kisogoni.
Bageni: Mtukufu Jaji hapa zitampiga hapa,alisema Bageni akionyesha sehemu za begani.
Jaji:Umesema ulipelekewa maganda ya risasi baada ya siku tatu, nne je uliuliza kuwa maganda hayo waliyapata wapi?
Bageni: Niliuliza wakasema waliyatoa Sinza eneo la tukio.
Jaji:Waliya-collect siku hiyohiyo?
Bageni: Nadhani maana askari akipiga risasi lazima a-collect maganda.
Jaji:Kama pale ukutani kulikuwa na matundu sita na walikuletea maganda tisa je haya matatu uliuliza waliyatoa wapi?
Bageni: Ni kawaida Mtukufu Jaji kuwa unaweza kulenga risasi ikapita juu ya kitu ulichokusudia.
Jaji:Kwa maelezo ya James (mkuu wa upelelezi kituo cha Urafiki) ni askari wangapi waliopiga risasi siku hiyo?
Bageni: Hakunieleza ni wangapi.
Jaji:Balistic (Mtaalamu wa masuala ya silaha na milipuko) alisema ni silaha mbili tu ndizo zilizopia ya Saad na ya mshtakiwa wa 12 ,una ‘comment’ yoyote kwa hilo?
Bageni: Mtukufu Jaji, yeye ndiye mtaalamu.
Jaji:Umeeleza kuwa mshtakiwa wa kwanza alikushauri lini mbadili taarifa ya kwenda kwenye Tume ya Kipenka?
Bageni: Mtukufu Jaji, sikuwa specific katika tarehe ila rekodi isomeke siku ambayo alikuwa ‘summoned’ kwenye tume.
Jaji:Kwa nini alikwambia uandike nyingine wakati ulikwishaandika taarifa ya kwako?
Bageni:Aliniambai ifanyiwe marekebisho kidogo ili mambo yawe sawa.
Jaji:Mshtakiwa wa kwanza alisema hapa kuwa polisi hutii amri halali tu je hiyo ilikuwa ni amri halali?

Bageni:Ni halali sababu yeye ni mkubwa wangu
Naye Makelle, mkuu wa zamani wa upelelezi wa kituo cha Polisi cha Urafiki, alikana kuhusika na mauaji ya wafanyabiashara hao ingawa alikiri kuwa alifika katika eneo la tukio hilo wakati wafanyabiashara hao wakikamatwa.
Akielezea jinsi anavyolifahamau tukio hilo, Makelle alidai kuwa aliopata taarifa akiwa kituoni kwake alipata taarifa kutoka kuwa kuna tukio la unyang'anyi limetokea katika Barabara ya Sam Nujoma na kwamba gari la Kampuni ya Bidco limeporwa pesa na kutakiwa kufuatilia majambazi hao.
Mahojiano kati ya Makelle na wakili wake Magafu yalikuwa kama ifuatavyo.
Wakili: Shahidi, hebu ieleze mahakama unafahamu nini kuhusu mashtaka haya unayokabiliwa nayo.
Shahidi: Ilikuwa ni saa 12.30 jioni siku hiyo nilikuwa kituoni kwangu nikiwa kwenye kantini nyuma ya kituo hicho.
Wakili: Kulitokea nini?
Shahidi: Control room walitangaza kuhusu tukio la uporaji katika Barabara ya Sam Nujoma.
Wakili: Baada ya taarifa hiyo ulichukua hatua gani?
Shahidi: Control room aliniita mlinzi moja tano nane
Wakili: Hiyo ndio kosaini yako?
Shahidi: Ndio.
Wakili: Walikueleza nini?
Shahidi: Walinieleza kuwa kuna tukio la robbery Sam Nujoma na kwamba kwa maelezo ya askari walikuwa wamefika kwenye eneo la tukio, walisema majambazi waliohusika na uporaji huo wameelekea Sinza na Kijitonyama. Hivyo walinitaka nifuatilie maeneo hayo kama naweza kuwaona wakibadilisha namba.
Wakili: Baada ya kuitwa ni hatua gani ulichukua?
Shahidi: Nilikuja kituoni ili kuchukua gari na askari, lakini nilipata shida kidogo kwa sababu askari wa CID hawakuwepo.
Wakili: Ulifanyaje ?
Shahidi: Nilichukua askari wawili wa uniform (CRO), nikawaeleza kuwa kuna tukio la uporaji limetokea naomba tuongozane ili kufanya ufuatiliaji.
Wakili: Ni nini kilichofuatia?
Shahidi: Nilipanda kwenye gari nikaondoka kuingia Barabara ya Morogoro, mara nikawaona askari wa CID.
Wakili: Walikuwa ni akina nani hao askari wa CID uliowaona?
Shahidi: Walikuwa ni mshitakiwa wa 10, Koplo Abinet Saro na WP Jane mshitakiwa wa tano.
Wakili: Baada ya kuwaona ulifanya nini?
Shahidi: Nilisimamisha gari nikawaambia wale askari wa uniform wateremke nikawaamuru askari wa CID waingie na nikawaeleza kuwa kuna tukio hilo na kuwaambia wakiona gari lolote limeegeshwa, wawe makini.
Wakili: Mlielekea wapi?
Shahidi: Tuliingia Morogoro Road, tukaenda mbele kidogo tukaingia kulia Barabara ya Shekilango. Tulipofika Shule ya Msingi Mugabe niliendesha polepole ili kufuatilia kwa umakini. Wakati huo ‘radio call’ yangu alikuwa nayo Koplo Abineth na WP Jane alikuwa amekaa nyuma.
Wakili: Wakati huo ni nani alikuwa akiendesha gari lako?
Shahidi: Ni mimi mwenyewe
Wakili: Baada ya kuendesha mlifika wapi na ni nini kilichotokea?
Shahidi: Tuliingia kulia kuna barabara tukawa tunaelekea Mwenge, lakini kwenye vichochoro.
Wakili: Mlifika wapi?
Shahidi: Mbele kidogo tuliona kundi kubwa la watu wakiwa wamesimama.
Wakili: Muda huo ilikuwa ni saa ngapi?
Shahidi: Ilikuwa inakaribia saa moja lakini bado kulikuwa na mwanga wa jua.
Wakili: Ni ni kilifuata?
Shahidi: Askari waliniuliza kuna nini pale lakini nikawaambie kuwa ngoja kwanza tusogee. tulipokaribia niliona askari mmoja akiwa amevaa uniform akiwa na bunduki ya SMG mkononi, akanisimamisha.
Wakili: Ulisimama?
Shahidi: Nilisimama na kuteremka kisha nikajitambulisha.
Wakili: Uliposimama na kujitambulisha, huyo askari aliyekuwa na uniform alikueleza nini?
Shahidi: Alinieleza kuwa walikuwa wakifautilia tukio la uporaji wa pesa za Bidco lililotokea Sam Nujoma.
Wakili: Walikueleza kitu gani kingine?
Shahidi: Walisema walipofika hapo wakiwa kwenye gari aina ya Pickup waliona magari mawili yamesimama. Gari moja lilikuwa jeupe lilikimbia na watu watu wanne walikimbia na kuingia kwenye gari lingine lenye rangi ya ‘dark blue’, ambalo ‘walili-block’.
Wakili: Ulichukua hatua gani tena?
Shahidi: Nilisogea karibu nikakuta askari nikawauliza vipi, wakanijibu kuwa wanawa-suspect kwa kuwa wamewakuta na bastola na wana pesa ambazo wanababaika hawajui idadi yake lakini wanakadria kuwa ni Sh.5mil.
Wakili: Kwa nafasi yako, uliwaelekeza nini?
Shahidi: Niliwashauri kuwa si vizuri kukaa nao kwenye mkusanyiko wa watu wengi nikaambia wawachukue na kuwapeleka kituoni ili kuwafanyia mahojiano na kama watakuwa na hatia basi hatua nyingine za kisheria zichukuliwe.
Wakili: Hiyo Pickup uliyoikuta ilikuwa ni ya wapi?
Shahidi: Ilikuwa ni ya kituo cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, japo haikuwa na maandishi lakini niliweza kuitambua sababu mara nyingi Afande Masinde (aliyekuwa mkuu wa kituo hicho) alikuwa akiitumia.

Wakili: Yule askari aliyekuwa na uniforn na SMG aliyekusimamisha naye yuko hapa?
Shahidi: Kwa sasa hayupo, ila tulikuwa naye.
Wakili: Alikuwa ni nani?
Shahidi: Alikuwa ni Nyangelela (mshtakiwa wa sita aliyeachiwa huru)
Wakili:Askari wengine waliokuwa wametoka Chuo Kikuu walikuwa ni wangapi na ni akina nani?
Shahidi: Kulikuwa na wenye uniform na wasio na uniform idadi yao siikumbuki lakini hawakuwa wengi sana.
Wakili: Kuna mshitakuwa yeyote uliyem-identfy pale siku hiyo?
Shahidi: Ndio, yule aliyeendesha pickup alikuwa ni mweupe na mnene.
Wakili: Alikuwa ni nani?
Shahidi: Alikuwa ni Noel (mshitakiwa wa nne ambaye pia aliachiwa)
Wakili:Ulielekeza nini kifanyike juu ya zile pesa na bastola ilioyokamatwa?
Shahidi: Askari wale walitaka kumkabidhi WP Jane, lakini mimi nikakataa na kuwaambia waondoke nazo na bastola kwa sababu hicho ni kielelezo.
Wakili:Ni maelekezo gani mengine uliyoyatoa?
Shahidi:
Niliwaelekeza waende kituoni kwa ajili ya kuwafanyia mahojiano.
Wakili: Wapi?
Shahidi:Kituo cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Wakili:Eneo la Sinza liko chini ya mamlaka gani?
Shahidi: Pale ilikuwa ni wilaya ya Kinondoni.
Wakili :Ni jambo gani jingine ulifanya?
Shahidi : Askari waliwachukua watuhumiwa wakawaweka kwenye pickup na askari aliyenisimamisha akapanda kwenye lile gari aina ya saloon
Wakili :Wewe na askari wako mlienda wapi ?
Shahidi: Nilirudi kwenye gari langu ambako Koplo Abineth alikuwa amebaki kwenye gari.
Wakili: Abineth alikuwa na silaha?
Shahidi: Askari wa CID huwa wanakuwa na silaha na yeye ndo alikuwa incharge wa kikosi cha doria.
Wakili: Na WP Jane alikuwa na silaha?
Shahidi: Hapana hakuwa nayo.
Wakili:Baada ya kutoka pale ulielekea wapi?
Shahidi: Nilichukua redio yangu nikawajulisha Control room nilichokuwa nimekishuhudia kuwa askari wa chuo kikuu wamekamata majambazi wanne wakiwa na bastola na pesa zinazokadiriwa kuwa Sh.5mil.
Wakili: Ulijibiwa?
Shahidi: Ndio, aliuliza kama ninao nikamwambia kuwa wameondoka nao na kosa laao siijui.
Wakili: Wakati huo ilikuwa majira ya saa ngapi?
Shahidi: Ilikuwa majira ya saa moja, lakini bado kulikuwa na mwanga wa kutosha.
Wakili: Ulipotoka pale ulikwenda wapi?
Shahidi:Nilikwenda kuwadrop askari wangu Ubungo Terminal ili waungane na wenzao kwenye doria.
Baada ya hapo nilielekea Ubungo Maziwa hadi Chuo cha Usarishaji.. kuna kituo cha polisi pale na nilipotoka pale niliendesha polepole kuelekea kituoni kwangu.
Wakili:Ni wakati gani ulipofika kituoni hapo?
Shahidi: Ilikuwa ni kwenye saa 1.30 hivi.
Wakili:Baada ya kufika kituoni ni jambo gani jingine lilitokea?
Shahidi: Nilimkuta OCD (mkuu wa polisi wa wilaya) wa Magomeni SSP Mantage akiwa amekaa nje pembeni kabisa kwenye kiti.
Wakili: Mlisalimiana? Tulisalimiana, nikamuuliza kuwa mbona leo uko huku akanijibu kuwa namsubiri afande nimkabidhi vielelezo.
Jaji Salum Massati: Afande gani?
Shahidi: Hakumtaja jina
Wakili: Alipokueleza hayo kilifuata nini?
Shahidi:Nilienda ofisini kwangu na baada ya dakika kama 20 nilitoka nje nikaongea na askari wa zamu CID.
Wakili: Baadaye kilitokea nini?
Shahidi: Nilimuona Matage akiwana SP Mkumbo, mshtakiwa wa pili SP (Christopher Bageni) wakaingia ofisini kwa OCS. (Mkuu wa Kituo) ASP Juma Ndaki. Niliwafuata na kwa kuwa viti vilikuwa vimejaa, nikasimama mlangoni
Wakili: Ni nini kilizungumzwa?
Shahidi: Matage alinituma nikalete mkoba kutoka CRO.
Wakili: Huo Mkoba ulijua ulikuwa na nini? Sikuwa ‘aware’ (sikufahamu), lakini waliniambia tu kuwa chukua vielelezo.
Wakili:Sasa umefikisha huo mkoba kwa Ndaki, nini tena kiliendelea?
Shahidi:Nilimkabidhi OCD akafungua na kutoa pesa na bastola
Wakili: Zilihesabiwa?
Shahidi: Ya OCD alihesabu na tukaangalia.
Wakili:Zilikuwa kiasi gani?
Shahidi: Zilikuwa Sh.2.7mil na kitu.
Wakili:Baada ya kuhesabiwa ni maelekezo gani yalitolewa?
Shahidi: OCD alimkabidhi mshitakiwa wa pili. Lakini mshitakiwa wa pili alionyesha ‘ku-resist’ kuzipokea akisema kuwa hakuagizwa kuchukua kiasi hicho.
Wakili:Baada ya mshitakiwa wa pili ku-resist wakubwa waliokuwepo pale walichukua hatua gani?
Shahidi: Mantage alimuita mlinzi mbili ambaye alikuwa ni RCO na kaimu kamanda ambaye ni mshitakiwa wa kwanza (Zombe)
Wakili: Mlinzi mbili aliitikia
Shahidi: Ndio, alikuja akatukuta tunamsubiri.
Wakili: Alipofika mlinzi mbili alifanya nini?
Shahidi: Alichofanya ni kufoka hakutusalimia na hata ile shikamoo yangu hakuipokea. Alifoka kuwa kama mmeshindwa kazi nataka pesa kesho zitimie, alifunga mlango na kuondoka.
Wakili: Naye hakuridhika pesa kupotea aliona kuna uzemba, je alipoondoka Matage alichukua hatua gani?
Shahidi:Alimkabidhi mshitakiwa wa pili akapokea na kuondoka na mkoba ule.
Wakili: Kati ya hao wakubwa waliokuwepo hapo kuna yeyote aliyewahi kukuuliza tukio la Bidco?
Wakili: Unakumbuka suala la Bidco limeibuka lini hadi leo uko hapa mahakamani?
Shahidi: Kwanza tarehe 16 mwezi Januari nilisoma kwenye magazeti kuwa waliouawa si majambazi na kilichonistua ni kuona kuwa ni wa tukio la Bidco, ndipo nilipostuka kuwa kumbe walikamatawa wakapigwa risasi tena.
Wakili: Uliwahi kuitwa kwenye timu ya IGP(mkuu wa polisi)
Shahidi: Sikuwahi kuitwa
Wakili: Jana mshitakiwa wa pili alionyesha hapa mahakamani kuwa uliwahi kuitwa na kuandika statement yako (maelezo) je unasemaje?
Shahidi: Sijawahi kuitwa na bahati nzuri ACP Mgawe (Kiongozi wa timu) anaijua namba yangu lakini hakuwahi kuniita.
Wakili: Je uliwahi kuitwa kwenye tume aliyoiunda rais kuchunguza tukilo hili?
Shahidi: Sijawahi na wakati nilipoondoka kwenda Misri Tume iliuwa na siku tatu kwa hiyo nilitegemea kuwa mimi ndio nigekuwa wa kwanza kuitwa kuhojiwa, lakini hadi ninaletwa hapa sijawahi kuhojiwa.
Kwa ujumla unasema ni kuhusu tukio hilo”
Shahidi: Mtukufu Jaji na waheshimiwa wazee wa mahakama, kuna mchezo mchafu nimefanyiwa kwenye Tume ya Kipenka kuhusu document hizi. Ninahisi kuna kitu kwenye tume hiyo si cha kawaida hadi ninapigiwa simu nikiwa Misri kuwa ninahusika katika mauaji haya sikuwa najua chochote. Tukio la Bidco ninalifahamu kama nilivyolielezea na si mauaji haya.
Wakili: Kuna statement ya Rajabu (mshitakiwa wa 12 ) kuwa ulionekana kwenye eneo la mauaji. Unasemaje?
Shahidi: Mimi si miongoni mwao, kwanza sikumjua Rajabu hadi nilipomuona mahabusu nikawa ninawatania wenzangu kuwa mbona mmemleta hapa mganga wa kienyeji ndio wakaniambia kuwa huyo ni Koplo Rajabu maana alikuwa na madevu yamechoka sana.
Wakili: Unasemaje kuhusu maelezo haya?
Shahidi:Sijui chochote kuhusu hayo mauaji
Wakili: Mshitakiwa wa kwanza juzi alisema hapa kuwa ukiwa gerezani na wewe uliandika barua kwenda kwa DPP (mkurugenzi wa mashtaka). je unazifahamu?
Shahidi:Sijawahi kuandika barua kwa DPP.
Wakili:Mahakama iamini nini kuhusu tukio hili?
Shahidi: Mtukufu Jaji na waheshimiwa wazee wa Mahakama, umesikiliza ushahidi,wa upande wa mashitaka, umesikia maelezo yangu, binafsi,naomba mahakama itende haki kwa jinsi njilivyojieleza kwa tukio la Bidco na si kwa maujai haya.

Katika kesi hiyo Zombe na wenzake wanatuhumiwa kuwaua kwa maksudi wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Wilaya ya Mahenge mkoani Morogoro ambao ni Sabinus Sabinus Chigumbi maarufu kama Jongo na ndugu yake Ephrahim Chigumbi, Mathias Lunkombe Juma Ndugu,dereva teksiManzese jijini Dar es Salaam.
Mbali na Zombe washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni SP Christopher Bageni, ASP Ahmed Makelle, F.5912 PC Noel Leonard, WP 4593 PC Jane Andrew, D6440,CP Moris Nyangelela,CPL Emmanuel Mabula, E6712 CPL Felix Cedrick, D8289 PC Michael Sonza, D 2300CPL Ebeneth Saro, D.9312D/C Rashid Lema, D4656 C/CPL Rajab Bakari na D.1367 D/CPL Festus Gwabisabi.
Kesi hiyo iliahirishwa hadi leo itakapoendelea tana mahakamani hapo ambapo upande wa utetezi utatoa hoja zao.

No comments: