Tuesday, February 17, 2009

MNASHANGAA?

Jamani muda mrefu mzee Mkapa alikuwa hajaonekana mitaani, hata Sumaye lakini kikubwa alichotuachia ni uwanja mpya wa taifa kumbe hata yeye alikuwa hajauona? Cheki anavyoshangaa!!! Watanzania badala wamwache mzee wa watu ale uzee vyema wanamletea fitna!

2 comments:

Anonymous said...

uadilifu ndio kitu cha muhimu, lakini ukiwa mwizi na kuwaficha wezi wengine, hata mazuri mengine huwa hayaonekani, ninachojua pesa za kujenga uwanja huo zimetoka kwa walipa kodi wa Tanzania, yeye alikuwa ni kama ufunguo.

Anonymous said...

Mimi siyo jaji wa kumhukumu mtu yoyote na siyo mwezeshaji au muumba mbingu na ardhi, kwahiyo kuhusu ubaya wa mtu nitatizo la kila mwanadamu, mimi,wewe na nyinyi hatujijui makosa yetu na mazuri yetu lakini tunaweza kusema ni wema, lakini huyu mwanadamu baadae akajigeuka, namaanisha kujisahau lakini navyo jua kwa nchi kama yetu tunaweza kabisa kuendelea.
Nakubali kazi za viongozi wetu na waheshimiwa maraisi wote waliopita na pia Mheshimiwa DR Jakaya Kikwete. Kwani kazi ya serikari mimi navyojua bila ya sisi wananchi siyo rahisi kabisa basi na sisi wananchi bila ya kuwaonyeshea vidole hawa viongozi, kwanza mtu ujiulize umeifanyia nini nchi yako?
Hata kuzoa takataka kwenye mfereji uliopita mtaani kwenu, ni moja ya vitu vya kuzingatia na mengineo mengi tuu.
Tusiwe tunapenda kumwachia kila kitu Serikali kwani huyu serikari ni wewe na mimi na yule, au tuwe tunachonga tuu tuu hawa jamaa wezi kama mtu unauhakika(ushahidi) peleka malalamiko sehemu usika Dr Jakaya atashughulikia lalamiko lako.

Bila kusahau tuwe tunawapa heshima hawa viongozi kwani kuwa kiongozi siyo easy kama mtu unavyomchafua jina flani.

Kama msomi navyojua unatakiwa kumpa credits mtu akifanya jambo la maana na Mh, Raisi mstahafu Benjamini Mkapa na Cabinet yake wapewe HONGERA kwa STADIUM mungu akitujaria utasikia soon flani wa Bongo anchezea Chelsea, Man U na n.k ndipo faida za wanja letu. soka litaongezeka kiwango kwani material tunayo

Bila kusahau Wabongo mlio ughaibuni kumbukeni kununua flana za timu yetu ya taifa kwani hiyo itasaidia kuitangaza taifa letu.
Ni jukumu letu wote wananchi.Itachangia hata mama zetu kule vijijini kupata maisha bora kwa upande mwingine.

Ningependelea kuona vitabu vya viongozi wetu vinauzwa ili tuwe tunajifunza kama wananchi matendo ya viongozi na siyo kuona mtu yoyote kama mhandishi wa habari anajiandikia anakuwa anawadanganya wananchi kwani mengi wanayoyaandika huwa yanakuwa hayana vyanzo kamili.

Na kama serikari au kiongozi mwenyewe achukue jukumu la fedha zote za vitabu hivyo viwe vinakwenda kwenye wizara maalum kubail matatizo ya kitaani hii itachangia mtu kukumbukwa kwa mazuri sana.
Na kupunguza udaku wa wana habari wapotofu.

Mungu ibariki Taifa letu Tanzania, Mungu ibariki Africa

Mdau kutoka kitaani