Friday, February 13, 2009

NGOMA AFRIKA BAND







Ilikuwa majira ya saa sita za usiku,mtangazaji Edo Ndaki aka Masai,akiutangazia umati wa washabiki kuwa sasa wanapanda jukwaani "The Ngoma Africa Band" !shangwe! vifijo!na mayoe! vilisikika wakati kiongozi wa bendi hiyo maarufu Ras Ebrahim Makunja aka Ras Makunja "Bw.Kichwa Ngumu" akiongoza jukwaani kikosi chake cha "The Ngoma Africa Band" au kama wanavyojulikana kwa majina kama vile FFU, The Golden Voice Of East Africa,Wazee wa kuzuia rushwa n.k.
Ras Makunja akiiongoza jukwaani au ulingoni bendi
hiyo yenye utajili wa wanamziki mahiri waliobobea katika kucharaza vyombo wakiwemo yule mpiga solo gitaa machachari wa bendi hiyo Christian Bakotessa aka Chris-B,ambaye kila wakati alionekana kuwatia kiwewe washabiki na mio wa gitaa lake!
wengine waliokuwapo jukwaani ni pamoja na mwanadada Severn Nsiku ambaye alikuwa akienda sambamba na Ras Makunja katika kuwatia wazimu washabiki! Ras Makunja na bendi yake hiyo hilionyesha uwezo wake mkubwa kuwa dansi lao halina mpinzani,
Bendi maarufu kwa kuwadatisha hakili na kuwatia kiwewe washabiki barani ulaya imeudhihirishia umati washabiki kuwa kweli wa ni "Mzimu wa Mziki",
katika onyesho hilo la kufa mtu bendi ya "The Ngoma Africa" imejiwekea rekodi ya pekee nchini Finland,baadhi ya washabiki waliojiwa walihitaja bendi hiyo kuwa ni ya aina yake!
Haijawai kutokea bendi ya dansi ya kiafrika ambayo imefanikiwa kuwatoa jasho washabiki wakati huu wa msimu wa barafu hapa Finland!moja ya washabiki alidai!

Wengine waliitaja bendi hiyo kuwa ni "Mzimu"unaowapandisha mzuka kwa haraka washabiki!
Katika jambo la kufurahisha pale baadhi ya wasahabiki walishindwa kujizuia hisia zao na walipanda jukwaani kucheza !mojawapo walionaswa mzimu na kupanda mzuka ni bloger maarufu KIBUNANGO! wengine ni DJ maarufu JahGun-Bongo,wakina dada wa kifini nao walijumuhika jukwaani pamoja na walinzi kuwepo lakini washabiki waliwazidi nguvu walinzi,kama kawaida ya bendi hiyo kila inapotumbuiza lazima vituko kama hivyo vitakuwepo!
Kiongozi wa bendi hiyo Ras Makunja alionekana kuzongwa na washabiki kabla ya kupanda jukwaa kiasi hakuwa na njia ya kuwakwepa washabiki hao,kuanzia kwenye chumba cha kuvalia hadi jukwaani "Bw.kichwa ngumu"Ras Makunja kakumbana na washabiki wenye "Vichwa Ngumu"kama yeye,kama alipoulizwa anajisikia vipi? alijibu
"Poa tu" "mimi ni mtumishi wa watu" "kichwa ngumu + vichwa ngumu vya wshabiki"ni sawa sawa "Super power" makunja alijibu.
Bendi hiyo yenye makazi yake nchini Ujerumani hilianzishwa mwaka 1993 na kiongozi,mwimbaji na mtunzi Ebrahim Makunja aka Ras Makunja "Bw.Kichwa Ngumu"
ilianza na wanamziki wachache wakiwemo Saidi Jazbo Vuai,lakini sasa imetanuka na kufikia idadi ya wanamziki kumi wakiwemo Richard Makutima(Drum) ambaye anasaidiana na Willy,Maxim Buanda (bass)ambaye anasaidiana Said Jazbo Vuai pia anaimba,
Chris-B(Solo)Mwanadada Severn Nsiku ambaye anaimba na kucheza show na Bibie Baby ambaye anacheza show,Sele Juma,ndani (rhythim gitaa) kikosi hiko kikikamilika jukwaani hakuna jingine wanachokijua dhidi ya kuwadatisha hakili washabiki,kama anavyodai kiongozi wa bendi hiyo Ras Makunja "Jukwaa ni sawa na ulingo wa Nguumi" bora kwenda Draw na washabiki kuliko kupigwa K.O!
Ras Makunja na bendi yake "The Ngoma Africa Band" aka "The Golden Voice Of East Africa"aka FFU au MZIMU wamefanya kweli UFINI.

3 comments:

Anonymous said...

ngoma africa mziki wao umeenda shule,´vijana hawataki mchezo kabisa wakiwa jukwaani

Anonymous said...

wajama hawa mie nawasifu kwa kukomaa kichwa katika medani

Anonymous said...

hi!ras makunja na mzimu wa dansi!?naona kazi moja tu ya kutupa madongo!!!te!te! mpaka kieleweke