Saturday, February 21, 2009

UMASKINI

Mtoto aliyeuzwa na mamake apatikana Mtoto Fatma Kisawiro akiwa na Mama yake mzazi Tabu Wiliamu katika makao makuu ya jeshi la Polisi jijini Da r es Salaam jana


MTOTO anayedaiwa kuuzwa na mama yake amekutwa katika maeneo Chalinze akiwa hai na kwamba mtu anayedaiwa kumnunua mtoto huyo amekimbia.

Kupatikana kwa mtoto huyo ni matokeo ya bibi wa mtoto kutoa taarifa baada ya mtoto huyo kudaiwa kuuzwa na mama yake mzazi kwa mwanamke wa kimasai ambapo kwa kile alichodai kuwa kuwa ni hali ya maisha imekuwa ngumu na kwamba asingeweza kumtunza mtoto huyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Suleiman Kova alisema wamempata mtoto huyo Chalinze na kwamba aliyemunua ametoroka.

Mwanamke anayedaiwa kumuuza mtoto wake huyo mwenye umri wa miezi tisa, Tabu William (36), bado anashikiliwa na polisi katika Kituo cha Chang’ombe baada ya kupimwa kama ana matatizo ya akili ama la.

Tabu alipelekwa jana katika Hospitali ya Wilaya ya Temeke chini ya ulinzi wa polisi ambapo alipimwa na daktari wa afya ya akili hospitalini hapo, lakini hata hivyo majibu ya vipimo hivyo hayakufahamika mara moja kutokana na madaktari hao kugoma kutoa majibu kwa waandishi kutokana na maadili ya taaluma hiyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Emmanuel Kandihabi, alisema mama huyo anaendelea kushikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi.

Mwanamke huyo alikamatwa Jumamosi iliyopita nyumbani kwao Mtoni Kidande, baada ya mama yake mzazi aliyekuwa akiishi naye, Fatuma Ally (70), kuripoti kupotea katika mazingira ya kutatanisha kwa mjukuu wake huyo katika kituo cha polisi Chang’ombe
.

No comments: