Sunday, March 29, 2009

AJALI YA CHENGE

Marehemu Vicky Makanya! Yeye ndiye alikuwa akifahamiana na Chenge sana na kila alipokuwa Mwanza alipenda kuhudumiwa na mwanadada huyu ambaye alikuwa muhudumu Casino!
Marehemu Beatrice Costantine!
Kibajaji walichokuwa wamekipanda!
Mzee Chenge akiwa hajui la Kufanya baada ya ajali hiyo iliyowaua wanadada hao wa kutoka Mwanza kwa bahati mbaya yaani kizungu coincedence ni kwamba Mheshimiwa alikuwa anamjua mmoja wao huko Mwanza! kama Mungu kakuandalia mikosi ni MIKOSI tu!
SAKATA la ajali iliyohusisha gari la waziri na mwanasheria mkuu wa zamani, Andrew Chenge na bajaj na kusababisha vifo vya wanawake wawili, limeingia katika sura mpya baada ya wafiwa kudai kuwa mmoja wa marehemu hao alikuwa akifahamiana na Chenge.
Chenge ambaye bima ya gari lake ilikuwa imekwisha tangu Juni 6, 2007, aliingia matatani juzi alfajiri baada ya ajali iliyohusisha gari alilokuwa anaendesha mwenyewe kuwaua Beatrice Costantine ambaye ni mfanyabiashara wa Mwanza na Vicky George Makanya.
Wakizungumzakwa nyakati tofauti jijini Mwanza na baadhi ya ndugu akiwamo mama mzazi wa Vicky, walisema wanafahamu Chenge kuwa alikuwa akimjua ndugu yao Vicky.
Akizungumza nyumbani kwake Iloganzala ambako kuna matanga jijini Mwanza, Mama wa Vicky, Nadhifa Kambi alisema amesikitishwa na taarifa za upotoshaji zilizoeleza kuwa bintiye na rafiki yake walikuwa wakienda Zanzibar kwa ajili ya kufunga ndoa.
Mama huyo aliyapinga maelezo hayo na kufafanua kuwa wasichana hao walikuwa wakirejea Mwanza baada ya kutoka Zanzibar ambako walikwenda kununua vifaa vya saluni.
“Ajali hii inanipa mashaka makubwa kutokana na kupokea taarifa za kupotosha za kufunga ndoa," alisema.
Mama huyo alisema pia amepata taarifa kutoka kwa wafanyakazi wenzake na Vicky kuwa alikuwa akifahamiana na Chenge na kwamba kila mara alipokuwa akifika Hoteli ya Mwanza alikuwa akimtaka yeye tu ndiye amhudumie vinywaji.
Kwa mujibu wa mama huyo, hata yeye aliwahi kumsikia mwanaye kufahamiana na mbunge huyo na kwamba aliwahi kumtaka atoke nyumbani kwenda kumuhudumia siku ambayo hakuwa kazini. Vicky alikuwa mfanyakazi wa hoteli hiyo katika kitengo cha King Casino ambayo kwa sasa inaitwa The Stone.
Ameiomba serikali kufanya uchunguzi wa kina ili kupata nini kilichosababisha ajali hiyo.
Msemaji wa familia ya marehemu Beatrice (kaka wa marehemu), Andrew Costantine akiwa Kiseke kwenye matanga, alisema wanachofahamu wao ni kuwa dada yake amepatwa na ajali akiwa njiani kurejea katika JVL Hotel iliyoko Mwananyamala walikofikia, wakati wakitoka Oysterbay kuchukua mizigo yao kurejea Mwanza.
Alieleza kuwa tayari Beatrice na rafiki yake Vicky walikuwa wametoka Zanzibar walikokwenda kununua bidhaa na vifaa vya saluni ambavyo vimekutwa hotelini walikokuwa wamefikia.



7 comments:

davidmusika said...

akina dada hao walionekana kwenye club moja na mzee chenge usiku huo, na zaidi mzee chenge aliaga mkewe kwamba anakwenda dodoma kwenye vikao vya chama jana yake saa kumi nambili jioni.

Anonymous said...

ajali ngapi zilizowahi kutokea bila kuundiwa tume ya uchunguzi kwani hii ina nini? tena watu walikufa ni wawili tu! kule arusha,Tanga watu wangapi walikufa katika ajali na hatukusikia tume? kuna nini kinataka kufichwa hapa? kwanza kabisa inabidi chenge awe jela kwa kuendesha gari bila bima ya gari kwa miaka 2! ebu fikiria ungekuwa wewe unaedesha bila bima ya gari wacha kupata ajali? nahisi bado tanzania hatuna usawa!mbona yule kijana aliyemuua chacha wangwe hakupewa dhamana? au tuseme hao marehemu ndiyo walioua chenge katika ajili hiyo wangepewa dhamana? jamani lazima tutenda haki kwa kila mtanzania kwa vile ni haki ya mtanzania kuwa na haki katika nchi yake.kumwachia mzee chenge huru ni kuendeleza matabaka ya walionacho na wasio nacho.

Anonymous said...

kwanza nawapa pole ndugu wa wafiwa.lakini nami naungana na mdau hapo juu. hivi kuna nini katika ajali hii mpaka tyume iundwe haraka haraka. mbona kuna ajali nyingi tu, tena zinazouz watu wengi atujasikia tume ikiundwa? hivi mara ngapi madereva wa daladala wamefungwa. hivi mtanzania wa kawaida anaweza kutembeza gari kwa miaka miwili bila bima?
Tanzania hakuna usawa kabisa, mkubwa ni ruksa kuua ila mdogo cha moto lazima ukione.

Anonymous said...

Hiyo tume isiishie kuchunguza ajali tu. pia wajue ni kwa nini mh,alikuwa anaendesha gari kwa miaka miwili bila kuwa na bima? pia kuna tetesi kuwa hao wasichana waliokufa mmoja wao alikuwa ni mtu wa kalibu sana na chenge,ichunguzwe isije ikawa ni ajali ya kupangwa kwa madhumuni fulani.na pia tujue isije kuwa hao wasichana walikuwa hapa dar kwa mwaliko wa mh. chenge. pia miili ichunguzwe kuona kuwa walikuwa wametumia kinywaji kikali na mh. naye achunguzwe kama alikuwa amelewa.

Michuzi Jr 2 said...

hivi kuna kitu gani katika ajari hii??

maana hata huyo dereva wa hiyo bajaji hajulikani alipo.hebu tujuzane jamani kinachoendelea.

Anonymous said...

Haaaaa!!!!!!!!! hivi hao wakuu wanajihisi vipi?? maana wapi yule alompiga risasi dereva daladala na hakukuwa na kifungo bali ni kuachiwa huru kwa muuwaji (tetesi ni kwamba alikuwa mtu wa karibu na rais. hii haiingi akilini kabisa) na mambo mengi tu yanayo fanywa na wakubwa wa nchi. myonge ni myonge tu. yaani huwanapandwa na hasira mpaka kipindi kingine huwa nafikiria kujilipua bungeni. ni bora nchi iendeshwe kijeshi tu watu tujue moja.

Anonymous said...

wamesahau kosa la kuendasha bila ya gari kuwa na bima(insurance au mzee vijisenti amemwaga vijisenti kwa kamanda kova na mwendasha mashitaka?tanzania kweli hakuna haki, jaribu wewe kuweka gari lako lisilo na bima utaona cha moto!!!