Wednesday, March 11, 2009

AKUDO IMPACT

KAMPUNI ya Bia ya Serengeti, SBL imeipa bendi ya Akudo Impact basi lenye thamani ya Shilingi 40 kwa ajili ya kufanyia shughuli mbalimbali za bendi hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya SBL, Jaji Paul Bomani alisema kuwa kampuni yake imetoa basi hilo kwa ajili ya kuwarahisishia shughuli zao mbalimbali za kufanya kazi yao.
"Tunataka kuona wanafanya kazi zao kwa ufanisi, hawa ni wajasiriamali wamemua kujiajiri kwa njia ya sanaa, sasa sisi kama SBL tunawawezesha.
"Hii itawafanya waweze kwenda popote pale wanapodhani kuwa wanafanya maonyesho yao kwa mafanikio na hakutakuwa tena na tatizo la usafiri," alisema Bomani.
Naye Afisa Uhusiano wa SBL, Teddy Mapunda alisema kuwa basi hilo litahudumiwa na kampuni yake wakati litakapokuwa likifanya shughuli za kupromoti bidhaa za SBL.
Akiishukuru SBL, Meneja fedha wa bendi hiyo, Adam Bundala alisema msaada wa kampuni hiyo umekuja kwa wakati mwafaka na kwamba basi hilo litasaidia kurahisisha shughuli za bendi hiyo.

No comments: