Thursday, March 12, 2009

ALIYEMZABUA MWINYI KORTINI

Ibrahim Said akiwa katika mahakama ya Kisutu leo alikokwenda kujibu mashtaka ya kumshabulia Rais Mwinyi. alichanganywa na wachina sijui waphilipino lakini watu waliokamatwa wakiiba samaki katika bahari ya Tanzania.


Kijana Ibrahim Said (26) amefikishwa mahakamani leo kwa kumpiga kibao Rais Mstaafu, Alhaj Ali Hassan Mwinyi.
Taarifa za polisi zinadai kuw amtuhumiwa huyo alipohojiwa alisema; kwa kitendo alichofanya, amefikisha ujumbe wake wa kuchukizwa na maelezo ya kuruhusu matumizi ya kondomu.
Hata hivyo, kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, mtuhumiwa huyo anadaiwa kusema kuwa anajutia kitendo hicho kwani hakukusudia kumpiga Mzee Mwinyi kwani anampenda.
Kamanda Suleiman Kova aliwaeleza waandishi wa habari jana kuhusiana na tukio la Mzee Mwingi (maarufu kama Mzee Ruksa) kupigwa kibao na kijana huyo juzi akiwa anahutubia Baraza la Maulid wakati wa kuadhimisha sikukuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) lililohudhuriwa na waumini wengi wa dini ya Kiislam katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.
Kamanda Kova alisema mahojiano na mtuhumiwa huyo aliyafanya mwenyewe juzi usiku na kumweleza kuwa hakuwa na nia ya kumdhuru, bali alitafuta kioja cha kufanya ili ujumbe wake wa kutaka viongozi wa dini wasisitize matumizi ya kondomu kwa waumini wao pamoja na kutoshabikia umoja katika kusherehekea sikukuu za Idd, Maulid, Pasaka na Krismasi.
“Mtuhumiwa huyo alisema viongozi mbalimbali wa dini waache kusisitiza matumizi ya kondomu kwani si njia sahihi na ni batili na potofu katika maadili ya kidini,” alisema Kova.
Hata hivyo watu mbalimbali walipinga kitendo cha kijana huyo kumpiga mzee Mwinyi kutokana na umaarufu wake na hata maadili aliyoonyesha wakati wa uongozi wake, ingawa baadhi walidai kuwa alikosea kusema juu ya kondomu kwenye hadhara ya waumini wa dini ya kiisilamu ambayo inakataza watu kufanya uzinzi.
Kamanda Kova alifahamisha kwamba, alipomhoji zaidi mtuhumiwa huyo kwa nini hakutafuta njia nyingine ya kufikisha ujumbe wake tofauti na kumchapa kibao; alisema alifanya hivyo kwa kuwa Mwinyi ni kiongozi anayependwa na kuheshimika zaidi hivyo kuamini kuwa kwa kufanya hivyo ujumbe wake utafika.
Akimnukuu kijana huyo Kova alisema: “Najuta kutenda kosa hilo kwa kuwa nampenda Rais Mwinyi, lakini ni njia sahihi ya kufikisha ujumbe huo,” alisema.

1 comment:

chalii said...

Kama kuna watu wanaostahili pongezi kubwa nchini Tanzania bac wa kwanza ni kijana Ibrahim aliyemzabua mzee ruksa mbao huo.kwani ni kama kamzabua kwa niaba yangu na kwa niaba ya watu wote waliokuwa kinyume na uzinzi.
Yaani mzee ruksa bado zile fikra kuruhusu ruhusu mambo hivyohovyo pasina kutumia sutaili ya akili! ianauma kwa kiongozi kama yeye kuwa na fikra ya kuruhusu condom,baada ya kuwaambia wananchi kwamba bwana acha tabia uzinzi kwa sababu uzinchi unathari kadha wa kadha ukiwemo ukimwi,yeye anawambia tumia condom,yaani suala la mwinyi ni kama jamaa flani aliyetaka kumuokaa jamaa yake aliyemkuta akifanya maandalizi ya kujidhuru kwa panga.akamwambia taafadhari sana ndugu usitumie panga hili kufanya hivyo sababu utadhurika sana, badala yake akampatia kisu na kumruhusu ili aendelee na maandalizi yake ya kutaka kujidhuru.
kufanya uzinzi bila condom ni sawa na kujiua kwa panga, na pia kufanya uzinzi kwa kutumia condom ni sawa na kujiua kwa kisu.
Pili ni kwamba ile ilikuwa ni siku maalum ya kuzaliwa kwa mtume (s.a.w) unapokaribishwa katika hafla kama hizo inatakiwa uje na maudhui inayohusiana na hafla yenyewe,ya nini kuzungumzia masuala ya kutumia condom mbele ya watu waliokusanyika kusinyika ili kujikumbusha mazazi ya Mtume wao kipenzi.au Mwninyi aliambiwa waislam wanafanya uzinzi biala kutumia condom,kwanza mzee ruksa inatakiwa apelekwe mbele ya sheria kabla ya kupelekwa mheshimiwa Ibrahim, sababu kitendo chake alichokifanya cha kutaja neno condom mbele ya waumini wenye heshima zao si kitendo cha ustaraab ni kuwazalilisha waislaam.
Mwisho ni kwamba,ikiwa mzee mwinyi ana kweli ana busara inabidi akae chini then atafakari,je ni kweli mimi nilikuwa katika haki kutaja taja misuala ya condom katika sikukuu za kuzaliwa kwa mtume wa Waislam au la? ikiwa kakosea; kama kuungama dhambi zake inabidi atoe amri ndugu Ibrahim arudishe uraiani.La sivyo ajue kwamba Ibrahim atafungwa hapa duniani lakini kesho akhera atakuwa sehemu nzuri akila matunda na maziwa kama malipo ya kumzabua mzee mwinyi.Ni mtzamo wangu jamani,kama ninakosea bac makosa hayo niachie mie.