Umati huo ulionekana kuwa na shauku kubwa ya kumuona mbunge huyo wa Jimbo la Bariadi akitinga kwenye mahakama hiyo baada ya gari aliyokuwa akiiendesha kugonga pikipiki ya matairi matatu na kuua wanawake wawili waliokuwa kwenye chombo hicho, maarufu kama bajaji.
Chenge, ambaye katikati ya mwaka jana alilazimika kujiuzulu wadhifa wake wa Waziri wa Miundo Mbinu baada ya kutajwa kwenye kashfa ya ununuzi wa rada, alitinga mahakamani hapo akiwa kwenye gari ya polisi, maarufu kama "rangi mbili" majira ya saa 5:45.
Alionekana kujiamini wakati akishuka kwenye gari hilo, huku watu wengi, wakiwemo wapiga picha wa magazeti na televisheni wakipigana vikumbo.
1 comment:
Dah Mrocky picha ya mwanzo amejikunja ili kupata nafasi amweke mzee sentzi katika lensi
Post a Comment