Tuesday, March 31, 2009

CHENGE KORTINI

Bw Chenge akiingia viwanja vya mahakama ya Kinodoni huku akilindwa na Polisi akiwamo Solomon aliyepata cheo kwa kupambana na majambazi wa Ubungo.
Sajini Solomoni akiwa na bisi wake RTO wa Kinondoni baada ya kumleta Chenge kortini.

Waandishi wa habari wakiminyana kujaribu kusikilizia kesi nje ya chumba ch amahakama kutokana na kufurika.
Wananchi wakiwa nje ya Mahakama hiyo.UMATI mkubwa wa watu jana ulifurika mahakamani kushuhudia kigogo akipanda kizimbani wakati waziri na mwanasheria mkuu wa zamani, Andrew Chenge alipopanda kwenye kizimba cha Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kujibu mashtaka matatu, yakiwemo mawili ya kusababisha kifo.
Umati huo ulionekana kuwa na shauku kubwa ya kumuona mbunge huyo wa Jimbo la Bariadi akitinga kwenye mahakama hiyo baada ya gari aliyokuwa akiiendesha kugonga pikipiki ya matairi matatu na kuua wanawake wawili waliokuwa kwenye chombo hicho, maarufu kama bajaji.
Chenge, ambaye katikati ya mwaka jana alilazimika kujiuzulu wadhifa wake wa Waziri wa Miundo Mbinu baada ya kutajwa kwenye kashfa ya ununuzi wa rada, alitinga mahakamani hapo akiwa kwenye gari ya polisi, maarufu kama "rangi mbili" majira ya saa 5:45.
Alionekana kujiamini wakati akishuka kwenye gari hilo, huku watu wengi, wakiwemo wapiga picha wa magazeti na televisheni wakipigana vikumbo.









1 comment:

Anonymous said...

Dah Mrocky picha ya mwanzo amejikunja ili kupata nafasi amweke mzee sentzi katika lensi