Wednesday, March 25, 2009

KANDORO KABANWAJamani kazi ya uongozi ngumu, cheki wakazi wa Kata ya Kipawa walivyokomalia mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Abass Kandoro kuwa hawamtaki mkuu wao wa wilaya, Patrick Tsere kwa madai kuwa ameshindwa kushughulikia madai yao na kutaka eneo hilo litangazwe kuwa "janga la kitaifa".
Wakazi hao, ambao jana waliandamana hadi ofisi za Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) zilizo Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, wanaishinikiza serikali kuwalipa fidia baada ya kuzuiwa kuendeleza makazi yao kwa takriban miaka 12 kwa sababu za upanuzi wa uwanja huo.
Wakazi hao walikuwa wamebeba mabango yenye ujumbe kama "Rais na Waziri Mkuu ogopeni Mungu kwa kutuwekea alama za X, wajabika" na mwingine uliomtaka Waziri wa Miundo Mbinu, Shukuru Kawambwa kutimiza ahadi zake na pia kumtaka mkurugenzin wa TAA, Prosper Tesha kujiuzulu kutokana na kuwasababisha usumbufu.
Kandoro, ambaye alienda eneo hilo kwa lengo la kuongea nao baada ya kutaarifiwa kuwa wakazi hao wameandamana, alikuwa ameambatana na Tsere kuwasikiliza, lakini akakumbana na kauli kali kutoka kwa wananchi hao.
Jamaa waliwahi Airport wakijua JK angepanda ndege kwenda Comoro kwa kupitia terminal One kumbe akatimukia terminal Two! Ndio maana kandoro akakutana na mabango ya Rais, hizi ndio kama za Mwinyi.
Cheki picha tu wananchi wakasononeka wakalaumu, akajibu baadae ikagoma ikabidi atafakari cha kufanya!

No comments: