Friday, March 13, 2009

KIDEO CHA MWINYIKwa wanaoshindwa kuona hapo juu wanaweza kuingia kwa kubonyeza LINK

9 comments:

Anonymous said...

acha ufala weweee sisi tunahitaji kuona kideo siyo kutonyesha picha, ufala wako utatufanya tusikutembelee tupe vitu laivu, utatuwekeaje picha ya mnato. Kiko wapi hicho kideo unachosema????????

Anonymous said...

Asalaam Aleykum Bwana Mpoki.

Kwangu imefunguka, lakini sioni kama ni "Kibao" Hii ni "Konzi ya Back Hander".

Kibao ni kumpiga mtu kwa Mkono/Kiganja/Mkono Uwazi, tena iwe Shavuni au Usoni. Tena unapo mchapa kibao ni kiwe kibao cha nguvu, na hapo huweza kikakubalika kama ni Kibao. Na sio Una m "Tap" mtu halafu unasema "Umempiga Kibao?

Ahsante Bro.

Bro Wa Malindi.

Nautiakasi said...

We anon wa kwanza unaonesha adabu zako fupi hazivuki hata urefu wa visigino vya miguu yako! Sasa kumtukana Mzee wa sumo yahusu nini?? Yaani ukaanza kuporomosha mitusi kwa matatizo ya computer yako...mbona sisi yafunguka vizuri tu, tena kwa resolution bomba hasa! Jifunze kuwa mstaarabu kama hukuzaliwa mstaarabu..!

Anon wa pili, na wewe walalamika nini? Vibao viko vya aina 2 kuna kibao cha kufunika na cha kufunuwa, hicho alichopigwa mwinyi ni kibao cha kufunuwa, sio konzi kama unavyodai, na kibao cha weza kuwa umepigwa usoni, begani, mgongoni kichogoni au hata makalioni..ilimradi tu kuwe na hali ya kupigwa kwa kiganja cha mkono. Na hilo ndilo lililotokea kwa mzee mwinyi.
Nampongeza mpigaji wa hichi kibao, anaesema huyu kijana ni mpungufu wa akili, basi aende yeye akipime zake. Kama utaangalia vizuri video hiyo utaona jisni kijana alivyotumia akili, ujanja na uwezo wa hali ya juu wakijasusi kuweza kulifikia jukwaa la waheshimiwa, tena kufanikiwa kumpiga kofi sehemu sensitive mzee mwinyi!
1. Aliweza kuihadaa hadhira wakiwemo Usalama wa taifa waliosomea kazi yao na wanaolipwa mishahara kwa kodi za watanzania, akaikaribia meza ya Muheshimiwa sana.
2. Alilenga kumzima kabisa mzee mwinyi kwa ku target kumpiga kwenye kichogo ambako ndio kwenye medula, ni rahisi sana mpigwaji kupoteza fahamu. Hafanyi hivi mpungufu wa akili.
3. Alipoona haipati sehemu hiyo alioilenga, alizuga kama anataka kumnong'oneza kitu sheikh gorogosi, ili aipate vizuri.
4. Alipomaliza kazi yake hakukimbia sababu angesababisha kushambuliwa kwa risasi, kama ujuavyo askari wa tz wanataka sababu tu kuuwa, yeye alilala chini mwenyewe.

Anonymous said...

Dear readers;

Mimi naona humu watu wote wanajifanya ni wajuaji.

Wewe nautiakasi unajifanya mchambuzi na mjuaji wa kukosowa wenzio na kujifanya unafahamu zaidi ya wengi.

Kwanza mpigaji hakulenga kumzima kabisa mzee Mwinyi, huo wako ni uzushi, wacha uzushiiiii!!!

Ukiangalia tukio lenyewe kabla ya kupigwa kibao Mwinyi alikuwa kaelekeza uso kule sehemu ambayo yupo yule kijana, na alipogeuka tu kuiangalia karatasi ndipo yule kijana akajivuta na kumlenga mkono wake kwa kutumia sehemu ya nyuma ya kiganja, yule kijana hakukusidiya kumdhuru, kama unavyosema wewe kwamba alitaka kumzima kabisa. Kijana alitaka kufikisha ujumbe kwa kutumia mkono wake.

Tabia mbaya ya kujifanya mjuaji, kwa kukosowa wenzio wakati wewe huna hunani na wala huongozi maneno mazuri tukaiona hikma yake.

Kijana huyo angekimbiliya wapi, kwa fikra zako???

Kwaheri nimeandika kwa ajili yako tu!!

Nautiakasi said...

Anon unaenikosoa naona macho yako yana matege! Au computer yako ni pentiun 2! Au unamatatizo mengine kwenye ubongo, amabapo hata tukikupa miwani ya kurekebisha hayo maengeza au tukinunulia laptop mpya HP yenye wondow Vista bado haitasaidia!

Hem iangalie vizuri hiyo video...

1.Jamaa anafika meza kuu

2.Mwinyi anamuangalia, alijuwa labda analetewa kimemo, lakini jamaa hamshambulii sababu target yake sio uso ni kwenye medula (kichogoni).

3.Jamaa anampoteza maboya Mwinyi,kwa kuzuga kama anataka kuongea na sheikh gorogosi na wala hakuja kwa ajili ya Mwinyi.

4.Mwinyi anarudisha macho na uso kwenye karatasi yake, aendelee kutangaza kondomu.

5.Katika uharaka wa ajabu jamaa anainuka kwa kibao cha kufunuwa, anampiga mzee mwinyi kichogoni.

6.Mwinyi anayumba, anapata kizunguzungu kidogo.

7.Jamaa anaondoka taratibu, kama ametoka kupokea cheti cha mfanyakazi bora vile, anasubiri waandishi habari wampige picha.

8.Usalama wanamfikia jamaa analala chini...

NB:1. Huyu jamaa kama angekuwa chizi, angefika tu jukwaani na kumshambuli, bila kumsubiri mwinyi ageukie karatasi wala asingewaza kumzuga vile.

2.Kama angekuwa chizi, hilo wazo ulilosema eti angekimbilia wapi, chizi asingekuwa na muda huo wakujiuliza angekimbia tu popote pale."Kwanini utumbo utupwe na wenyewe twalia ndizi??"

Anonymous said...

Asalaam Aleykum Bw Nautiakasi.

Ndugu naona unajikanganya, mara unasema kapigwa kibao kwa mkono wazi na usoni, na mara ya pili unasema kapigwa Kichogoni/Medula.

Kwa sisi Wazanzibari? Khasa wa Malindi? Kibao kinapigwa Usoni au Shavuni na sio kwenye Kichogo au Uchogo.

Wala Kibao hakipigwi kwenye Mgongo au Bega au Tumbo ndugu yangu.

Ukisema Kofi?? Hapo hujakoseya, kofi unaweza kupigwa mwilini au popote Pale. Upooo Hapoo? Kiswahili, Ndugu yangu.

Tizama tena hiyo Video, Kijana katumiya "Back Side" of the hand. Na hiyo inaweza kuwa ni hiyo "Konzi".

Hakupigwa kwa open hand kama unavyosema.

Ahsante tena na ninakushukuru kwa comments zako, nitaomba Jazba Punguza.

Nduguyo.

Bro Wa Malindi.

Nautiakasi said...

Bro wa Malindi nna was was na ukazi wako wa malindi, huenda wewe ni miongoni mwa wale walokuja zanzibar kwa sherehe za majahazi halafu hamjarudi tena kwenu! Sababu kiswahili hujui
1. Kupiga kofi ni kitendo cha kugonganisha viganja kwa nguvu
2.Kupiga konzi ni hali ya kukipiga kichwa kwa kutumia nakoz za vidole vya mkono vilivyokunjwa, kifupi ni ngumi ipigwayo kichwani(rejea kamusi yako ya kiswahili cha unguja), hivyo haiwi konzi kama hakujakusanyaika vitu viwili navyo ni hali ya kuepo kinganja kilichokunjwa na kichwa kilichopigwa! Alompiga mzee mwinyi hakukunja kiganja, alipiga kibao kwa waswahili wa zanzibar twaita kibao cha "kelbu wahed" au kibao cha kufunuwa! Kinamatusi zaidi ya kibao cha kufunika! Kwa weledi wa mambo wanajuwa...

NB:Bro wa Malindi unabahati, Yale mambo ya zamani malindi yamekwishwa, simba hadi kunywa chai nyama zipo kaziwacha, lakini usjali tutakupeleka mahonda kwenye kiwanda chetu cha sukari kule miwa tele kama huna kazi utapara miwa au Tutakupeleka pwani ya kiwengwa ukitamani pweza utachokolewa, kule pweza tele kwenye mawe ya barini!
Usiogope ni ukarimu wetu tu huo wazanzibar ukinunuwa vocha ya simu pia utasuguliwa hakuna tabu, na kama utatamani dafu ukishakunywa maji mwambie muuzaji tu utachokolewa! Jitahidi usiondoke zanzibar sherehe za majahazi zimeisha lakini za mwaka kogwa zaja, tutakupeleka makunduchi wende ukapikiwe mseto wa kunde kisha upakuliwe! Zanzibar hii njema kila kitu utafanyiwa...!

Anonymous said...

Ukiangalia vizuri kwa mtu anyejua sehemu za kichwa, pale alipopigwa Mzee Mwinyi ni sehemu hatari, mtu unaweza kufa bila maelezo!

Mwaka mmoja aliopata, ashukuru Mungu, lile ni shambulio, tena la kudhuru kwa kukusudia!

Nimeshangaa kusikia kapata mwaka mmoja, pale yake ingekuwa mitatu hadi mitano!

Anonymous said...

naona sasa unaingilia mambo ya TZ, kazi kweli kweli...