Tuesday, March 17, 2009

KOROKORONI

Baada ya Mzee Pinda kutembelea Jiji na kuona ongezeko la vibaka wanaovuta bangi mpaka kwenye ukuta wa ikulu sasa moto umewaka jijini wanakamatwa watu wote, wavute bangi (msuba), wakabaji ama wenye sura za kinomanona ni Cetral tu. Sasa zoezi lingepelekwa mpaka uswahilini nadhani watu tungelala walau kwa wiki moja! Sasa hawa si wangepelekwa geza ulole wakazalishe tu?

3 comments:

Anonymous said...

Duuh,

Hii kali. Sasa wale wanaovuta unga kwenye viota vya Upanga, Kariakoo, mahekaluni ya Mbezi Beach, Oyster Bay, Msasani na kwingineko nao watakamatwaje?

Hii inanikumbusha wakati nasoma shule ya msingi tulikuwa tunawaona mgambo na polisi wakiwakimbiza watu wasio na kazi mitaa ya Kisutu na Upanga huku Wahindi kibao wakiangalia tokea kwenye varanda na madirisha ya viota vyao. Haikutokea hata siku moja mgambo kwenda kugonga hodi na kuwauliza vitambulisho vya kazi Wahindi kwenye maghorofa ya mitaa ya Zanaki, Kisutu, Mrima, Jamhuri, Sewa, India, Mali, Makunganya, Libya, Posta, Mtendeni au mitaa yoyote ya Upanga.

Wasio na kazi wengine walikuwa wamerundikana kwenye nyumba za Waheshimiwa mashemeji, kaka, dada, baba mdogo, mama mdogo wajomba, shangazi, binamu na kadhalika huko mitaa ya Oyster Bay, Msasani na kwingineko. Lakini kamwe hawakuguswa na heka heka za vitambulisho za mgambo na polisi.

Hawa tumeshawahukumu kuwa vibaka na wavuta bangi. Kuna wala-unga na vibaka domestic mitaa ya ushuani. Wao wanakula nyunga kwa raha zao kwa fedha za ufisadi na wakizikosa wanakwapua cherehani, video, dvd, music system, mikufu ya mama, dola za mzee na kwenda kubwenga ili wapate vijisenti vya unga. Hawa Muheshimiwa Pinda kawawekea mkakati gani?

Zile ajira milioni mbili za Muheshimiwa Rais zinaanza lini? Zikianza hawa wapewe priority ya kwanza. Na yale mabilioni ya Muheshimiwa Rais yakiwafikia hawa jamaa tutakuwa tumekata mzizi wa mgogoro huu.

Anonymous said...

Sura ya "kinomanoma" hio kali

chib said...

Hii inanipa picha ya hapa Kigali, Rwanda. Mtu akionekana na macho mekundu, polisi humkamata na kumhoji, maana yake inaashiria anapuliza mtemba mkubwa au hakulala usiku akiwa katika pilika za kuandaa valangati kwa serikali au kwiba