Saturday, March 07, 2009

MAHAKAMANI WIKI HII


Wiki hii mambo yamekuwa kama kawaida watu wenye majina wanatinga tu mahakamani kwa wanayodaiwa kufanya. Kwanza, Nickson Mahanga mtoto wa Naibu Waziri wa Ajira ,kazi na Maendeleo ya Vijana,Makongolo Mahanga akisindikizwa na Askari kurudishwa rumande baada ya kusomewa mashtaka ya kumjeruhi Joseph Daudi kwenye baa moja huko Chanika nje ya Dar es Salaam.
Lakini kali zaidi ni ya Merey Balabou mmoja wa Mapedejee nchini, Mkurugenzi wa kuuza mafuta ya TIOT, wanaoimbwa kwa fedha za kutisha kumbe alikuwa na soo ya kuiba Barclays zaidi ya dola milioni 1.4. Sasa najiuliza huyu utajiri wake wa kurithi, kujituma, ama ndio deal kama hizi? tuache mahakama itatuamulia!

1 comment:

muhammedsamir said...

Haya ya kweli jamani. Banki ya kimaitaifa inatapeliwa kiholela. Hebu tupeni taarifa kamili.