Friday, March 06, 2009

WEMA SEPETU

Nimekuwa nagonjweka kwa siku kadhaa ndio maana sikuonekana hewani lakini leoi nimerejea tena. Samahanini sana kwa hilo lakini ni la kibinadamu zaidi malaria hata ukilala kwenye net utaumwa na mbu baa!!
Tuache hilo linalonisumbua ni jinsi watu wanavyomzungumzia Wema Sepetu, Miss Tanzania wa miaka ile na binti wa wazee wa kiafrika!
Watu wanadai mtoto amedata, wengine wanasema hana akili na wengine wanamuona mualifu kama walivyo wengine mara baada ya kuswekwa lupango. Yote mawazo ya watu.
Lakini baada ya kutolewa lupango kwa dhamana na mama yake mzazi, Wema alifanya jambo ambalo ndilo linanisumbua zaidi.
Alipotoka alihaha kumtamfuta mpenzi wake na kumkiss hadharani nakutaka kuondoka nae bila ya kushauriana na mama yake.
Sasa Swali ni hili:
1. Alitenda kosa ama alikuwa sawa kwani ni mtu mzima over 18 yrs?
2. Alionyesha daharau kwa mama yake aliyetoka nyumbani na kuwekeza fedgha zake ili binti asiumie segerea?
3. Ama tatizo ni mkanganyiko wa malezi ya ng'ambo na kiafrika?
4. Huyu binti wanasema kaharibika ni baada ya kushiriki mashindano ya Urembo ama hata kabla?
5.Wema anahitaji ushauri nasaha ama familia nzima kwa yote yaliyowakuta?
Nadhani pamoja na kuwa yatakuwa maisha binafsi ya mtu lakini ni vema tukajadili kama walimwengu kwakuwa kuna ule msemo, Asiyefunzwa na wazazi......

3 comments:

Anonymous said...

Kwanza pole sana kaka kwa kuuguwa malaria, Mungu akupe afya njema!

Pili ahsante kutupa nafasi kujadili walau kwa uchache juu ya hili sakata la Wema bint wa Sepetu, ingawa ni mambo binafsi lakini yeye tayari ni National figure, sababu alishawahi kukabidhiwa bendera ya Tanzania kwenda kuwakilisha taifa, hivyo chochote akifanyacho sasa lazima ajuwe kita reflect katika jamii ya watanzania, ndo maana anaitwa kioo cha jamii, inshort nafasi yake katika nchi nikubwa kuliko yako Mzee sumo (sababu yeye alishawahi kubeba bendera ya taifa)wajuwa wenye hadhi ya kutembea na bendera ya taifa ni watu wa namna gani..!

Baada ya utangulizi huo, kiufupi kinachotokea hivi sasa kwa familia ya Wema sepetu, hususan mama yake ni Matunda wa kile walichokipanda...! Ndo kuthubutu kusema kwamba wazazi wa wema sepetu, wanakumbuka shuka kumekucha!! Waswahili wasema Mchelea mwana kulia hulia yeye, na wakaongeza tena kusema samaki mkunje angali mbichi, ukimsubiri ashakauka utamkata tu! Wao walichelewa, tena wamechelewa sanaaaaa...Inaonesha hawakucheza nafasi yao vizuri wakati wa malezi, kama kweli walitaka mtoto wao akuwe kwa desturi za kitanzani, au wamechanganya malezi, halafu wanashindwa kukubaliana na matokeo ndo maana sasa wanahangaika. I mean kama walikusudia kumlea kwa mila za kimagharibi, basi wamepatia sana, na hawana sababu za kulalamika kwamba wema hana adabu! Laa walikusudia kumlea kwa mila na desturi za kitanzania, basi walikosea sanaaa! Ingawa ana miaka zaidi ya 18 kwa mila na desturi za kitanzania bado hana mamlaka ya kulala nje ya nyumba ya wazazi wake kabla hajaolewa, hana mamlaka kulala na mwanaume yoyote awe kanumba au jumbe! Sasa cha ajabu mama yake wema, alikuwa anaridhia wakati mwanane analala nje ya nyumba yake na Kanumba, lakini sasa sababu ana lala na Jumbe imekuwa nongwa, wote ni wahuni tu hakuna mume! Jee utaweza kweli kumkana bint yako ikiwa mwanzao ulikuwa wachekelea alipokuwa akilala na Kanumba? Kwani na Jumbe nae simwanaume tu?!
Lakini kwa mila za kimagharibi hilo ni jambo sawa na halina makosa kabisa, zaidi mama ana makosa (anajichanganya) kumwingilia uhuru wakuchaguwa bint yake!

Jengine kwa mtazamo wangu, bint yoyote awezae kuvuwa nguo zake, akatembea uchi (na kichupi tu) mbele ya kadamnasi (wake kwa waume), huyo kwa mtazamo wangu anamatatizo ya akili tayari, kwa hiyo wanaosema wema ni mgonjwa hivi sasa naona walichelewa sana, mimi nlimuona mgonjwa wa akili tangu siku nlipoona anapita na kichupi mbele ya akina Hashim Lundenga! Kwani kuna tofauti gani, wale vichaa wanaotembea na chupi tu bara barani na hawa ma miss wenu? Kwa matazamo wangu hawa mamiss wenu ni vichaa by professional ndo maana wanalipwa tofauti ni hiyo tu!

Ushauri:
Mama wema (na familia) maji yashamwagika, hayazoleki, muhimu kausha sakafu kwa tambara(deki) mtandike mkeka mkae...Nna maana mukubali matokeo, muacheni mtoto achaguwe anataka kuishi na nani, akiwa mla unga au mla ganja! Hiyo ndio njia ya maisha aloichaguwa, akiona haimfai atarudi kwenye njia inayomfaa! Muiteni Jumbe mumkabizi wema wake wakalishane nyama ya kasa!

Anonymous said...

Salaam!
Binafsi ninakubaliana kabisa na mtoa mada hapo juu (Nautiakas) kwa mawazo yake. Yote anayofanya huyu mtoto (na wengine wengi tu wanaodhani ndiyo "uzungu" kufanya wafanyayo) yanatakiwa yaangaliwe zaidi kutoka kwenye mizizi (familia) na si matunda.

Wazazi wa Wema (na familia yake) wana majibu tosha juu ya wapi walikosea na waTanzania wengine hata tuseme vipi haitabadili jambo. Ni imani yangu kuwa familia bado wanayo nafasi ya kubadili hali ilivyo kwa sasa.

Kama alivyosema mtoa mada hapo juu, haya mambo ya "miss this" "miss that" ni ujinga na urimbukeni tu. Ninaruhusu kuitwa "Old school", lakini haya si mambo ambayo jamii iliyostaarabika inatakiwa kuyaendekeza. Hii pia inajumlisha yale mambo ya Big Brother. Mimi huwa yananichefua sana.

Kwa kusema hivyo, iwapo Wema alikuwa na baraka za wazazi wake kushiriki huu ujinga wa "u-miss...", basi wazazi hao hao wana jukumu la kupiga deki uozo waliosababisha.....

Ninaomba kuchangia

Anonymous said...

mimi nasema tu kwamba kuteleza si kuanguka, wazazi wa wema wana nafasi nzuri tu ya kukaa na mtoto wao na kuzungumza na mambo yakawa mazuri, kwanza kabisa naona bado Wema hajakomaa kiakili, alafu ni mambo ya kitoto au kiswahili, mambo ya kuchukuzana sijui na shoga kwenda kulipiza kisasi mi hayaniingii akilini kabisa, ebu wazazi waombe Mungu sana kuhusu mtoto wao alafu, maana inaonekana Wema ana mapepo huyo, atafunguka kwa maombi tu. mi sijui wazazi wa wema ni imani gani lkn ishu kama hizi ushauri plus maombi, mi kwa kuwa najua power ya Mungu iliyopo kwenye maombi najitolea kuomba kwa ajili yake ili Mungu amfungue, maana nakumbuka mdogo wangu alikuwa haambiwi kabisa akasikia, ingawa familia tumelelewa maisha ya kitz na sio kizungu, kumbe yalikuwa mapepo siku liliposhushwa ombi barabara mtoto mapepo yakaanza kupiga kelele tukakemea mpk yakatoka na yalipotoka tu mpk leo mdogo wangu amekuwa msikivu na adabu sana. yani amebadilika kabisa.

BY MLOKOLE