Friday, April 03, 2009

KOPLO LEMA AFA


Shahidi muhimu katika kesi ya Zombe, Koplo Rashid Lema, kufariki dunia leo alfajiri, habari za kifo chake zimethibitishwa na magereza pia madaktati wa Hospitali ya Ocean Road alipokuwa amelazwa.
Koplo Lema ambaye alikuwa ni mshitakiwa wa 11 katika kesi hiyo inayomhusisha aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi( ACP) Abdallah Zombe na askari wengine 12, alifariki duni jana saa 10.00 alfajiri katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, alikokuwa amelazwa kwa matibabu.
Yeye ndiye alielezwa kuwa shahidi muhimu katika kesi hiyo na hivyo inaleta utata kwa upande wa mashitaka ambao waliomba kesi imsubiri shahidi huyo, na sasa hatunaye tena.
Swali ni kwamba kesi kubwakubwa kwanini mashahidi muhimu wanakufa??????

1 comment:

chib said...

Habari hii inasikitisha na kutisha pia. Hasa ukizingatia pia na ndugu yake Koplo Lema wa karibu sana naye ameuawa kwa risasi bila kuporwa chochote, na mkewe aliyekuwa naye kuachwa mzima, inatia shaka sana. Tunajiuliza kulikoni? Kesi ya akina Zombe ina walakin