Wednesday, April 01, 2009

MASKINI WEMA!!!


Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu ameendeleza vituko visivyokuwa na mwisho kufuatia jana kufunguliwa mashtaka mengine na kuswekwa rumande kwenye kituo cha Polisi cha Kijitonyama, jijini Dar es Salaam.
Wema pamoja na mpenzi wake, Jumbe wamefunguliwa mashitaka ya wizi wa televisheni, redio na microwave (inayotumika kuchemsha vyakula).
Habari ambazo Mwananchi imezipata zinaeleza kuwa Wema na Jumbe wamefunguliwa jalada namba KJN/RB/1977/09 linalohusiana na wizi huo na inaelezwa mrembo huyo alibeba vitu hivyo kutoka kwao na kupotea navyo kwa mpenzi wake huyo ambako alijichimbia kwa siku kadhaa.
Wema ambaye amekuwa akiibua vituko mfululizo, bado kesi yake ya kuvunja kioo cha gari la aliyekuwa mpenzi wake, mwigizaji maarufu, Steven Kanumba inaendelea katika Mahakama ya Kinondoni.
Jana asubuhi, mama yake pamoja na dada yake anayeishi Sinza walionekana kwenye kituo cha Kijitonyama kuhusiana na suala hilo na imeelezwa walikuwa wanataka waelezwe vilipo vitu hivyo ili wawatoe nje kwa dhamana.
Hivi karibuni, hali ya Wema ilionekana kubadilika baada ya mama yake kumtafutia kazi, lakini siku chache zilizopita tabia yake ilibadilika tena na kuanza kurejea usiku nyumbani katika eneo la Sinza jirani na Lion Hotel ambako ni nyumbani kwa dada yake anakoishi baada ya kuibuka kwa tafrani mahakamani siku alipowekewa dhamana mwezi uliopita.
Jumbe amekuwa akituhumiwa kumfundisha mrembo huyo kutumia dawa za kulevya na alishindwa hata kumwekea dhamana alipolazimika kulala mahabusu lakini alipotoka, mrembo huyo alimkimbilia na kumsahau hata mama yake aliyechukua jukumu la kumuwekea dhamana hiyo.

1 comment:

Anonymous said...

Mzee "Sumo"

Humpati mtu hapa kwa kamba hiyo, maana siku hizi Wabongo wako makini sana. Wanaijua siku ya "Wajinga" kuwa, ni Aprili moja.

Lete lingine, tutakusikiliza "Mzee". Lakini naye huyu Wema, asipowakomalia watu wa magazeti na blogs, mwisho wake watamfikisha pabaya. Habari ndiyo hiyo!!!

This Is Black=Blackmannen