Tuesday, May 26, 2009

AJALI YA MWAKYEMBE

Tume iliundwa kushughulikia ajali ya mwakyembe na ripoti yake imetoka kama mdau chini alivyozungumzia stori ya Tanzania Daima. Leo tena wamesema kuwa Mwakyembe alikuwa amelala kwenye gari na Lori halikumgonga. hii ndio ripoti ya Kitaalamu ya Kamanda Kombe.
1. Sasa Swali: Kama Mwakyembe alilala basi dereva aliyekuwa nae ndio atakuwa anajua hilo.
2.Tume haikumuhoji dereva wa Mwakyembe na kutaka akamatwe ashitakiwe!
3.Wanasema ni mwendo kasi kitu ambacho kinajulikana kwani huwezi kuovertake ukiwa spidi ndogo.
4. Tume imevunja rekodi ya tume zote nchini kwa kutoa taarifa siku hiyohiyo ya kazi. lakini ripoti inafananafanana na stori ya Tanzania Daima Jumapili.

Lakini kikubwa ni jana polisi huyu nae alisukumwa mtaroni na Lori jijini Dar es Salaam na akabaki analilia gari lake, sasa kupewa pande na Lori ni issue?

Nawasilisha!

6 comments:

Anonymous said...

Tume hii siyo professional wala haina powers za reasoning.Tume ya kufunika ukweli.Maswali haya iyajibu:

1. Kuna dereva wa lori amehusishwa na ''ajali'' hii katika maelezo ya dereva wa mbunge. Dereva wa lori 'kajitokeza' Tanzania Daima na maelezo yake na hajajitokeza Polisi na wala Polisi haimtafuti yeye wala lori lake. Kwa nini?

2. Kombe anamuonya mbunge asiszungumzie ''ajali'' kwenye vyombo vya habari, wakati Kombe mwenyewe anatoa onyo hilo na kuzungumzia mengi tu kuhusu ajali hii kupitia vyombo vya habari. Kwa nini asijionye mwenyewe kwanza?

3.RPC wa Iringa saa chahche tu baada ya ''ajali'' alizungumza na vyombo vya habari na kusema hakuna mkono wa mtu katika ajali hii na stori kubwa tu ikatoka The Citizen, kwa mfano. Je Kombe amemuonya RPC? Na wakati RPC anazungumza hata mbunge alikuwa hajachukuliwa maelezo yake!!!

4. Dereva wa lori nae 'aliyejitokeza' Tanzania Daima nae ameonywa asizungumzie ajali hii kwenye vyombo vya habari?

5. Kombe na tume yake wasitufanye watoto. This is a very cheap propaganda job they are doing

Anonymous said...

Hii tume ina spidi kweli, kuliko hata dereva wa Mwakyembe! Tume iwe na uangalifu isije ikasababisha ajali!! Polisi wangekuwa na spidi kama hii kuwashughulikia mafisadi sidhani kama hata mafisadi wangepata nafasi ya kutuhujumu.
Inaelekea kuna spidi ya kuwashughulikia kina Mwakyembe na dereva wake na kuwageuzia kibao na spidi ingine tofauti ya kuwashughulikia kina Ro..., Sai..., Man... na washirika wengine wa kifisadi.
Tuko macho Kombe tunakuangalia!!!

Anonymous said...

Kombe tuko macho tunakucheki hata kama viti vyetu tumelaza!!!

Anonymous said...

Dereva wa lori hana jina, hana picha lakini Tanzania Daima wanamjua na wanamhifadhi. Kombe wala hamtafuti huyo dereva wa lori au ndiye anamficha.Anajificha nini, alikimbia nduki kwenye tukio la ajali kwa nini? Kombe hana habari na maswali haya anakufa na mbunge na dereva wake tu na kufanya upolisi kwa PR- mbinu mpya kabisa ya bongo. Grow up, Kombe it will not work.

Anonymous said...

http://macedoniaonline.eu/content/view/4023/53/
Mungu ibariki Tanzania, Wabariki viongozi wake

Anonymous said...

hii picha sio gari ya mwakyembe kaka acha fix