Tuesday, May 12, 2009

USAFIRI KWA TAXI
Pamoja na ndoto za Rais wa zamani, Benjamin Mkapa na Waziri wake John Pombe Magufuri, ya kuhakikisha watanzania wanatembea kwa Taxi kutoka Ntwara hadi Bukoba. Mambo yamegoma, kama inavyoonekana magari yakiwa yamekwama katika eneo la Muhoro wilayani Rufiji.
Sehemu hii mbovu kilometa 60 unazipiota kwa saa mbili. Sehemu nyingine inakera ni baada y aManyoni kama unaenda Mwanza. Sasa tunajiuliza hii ilienda kasi kwa ajili ya magufuli ama Road Fund ilitumika zaidi kujenga barabara?


4 comments:

Anonymous said...

dah! mdau umenikumbusha mbali nilshawahi shuhudia mh. maghufuli aki wambia jamaa wabomoe barabara wajaze mawe chini wakati ujenzi unaendelea maana walikuwa wameboronga ila toka jamaa abadilishwe wizara imekuwa tofauti kabisa, nashukuru kwa kuliona hilo. ila siku akitoka wizara ya vitoweo ndio kesi ya wale samaki walokamatwa itaamuliwa.

ni hayo tu na naomba kuwasilisha.

Anonymous said...

Magufuli aliondoka na barabara zake. Katika miaka minne iliyopita hakuna barabara mpya zilizojengwa wala kukamilika.
Wakati huo huo kwa kila lita ya mafuta tunayonunua tunakatwa hela kwa ajili ya kuboresha bara bara.

Bongo Pixs said...

Hiyo miroli mizito ndo maana Ka-taxi kanapita bila wasi2.

Irene said...

Mweeee!!! Kweli taxi na bajaji zinapita bila shida tena ka bajai ikileta shida unashuka unakainua unakatoa pembeni kama siyo kujitwisha kabisa then unaendelea na safari. Haaaa haaaa Tutamkumbuka Magufuli Daima!!! Japo hata kwenye samaki anafanya vizuri ila hao samaki tusubiri hadith ingine ya kuwa gharama ya kuwastore imekuwa mabilioni au walioza tukawatupa. Huku ndo kukumbatia maji kama jiwe UJINGA!!!!!!