Monday, May 25, 2009

YA MWAKYEMBE


Mdau ameniwekea hii comment nikaona labda mjadili si maoni yangu! Lakini naona kuna suala hapa!

Kuna kampeni ya kupotosha ukweli kuhussu ile ''ajali''.
Kwanza mkuu wa polisi wa Iringa alishasema eti ilikuwa ajali ya kawaida huku akikiri kwamba uchunguzi unaendelea.
Pili blog ya Godwin ilishasema kwamba eti chanzo chja ajali ni shimo katika barabara mbovu ya Mbeya Iringa- lakini katika taarifa yake hiyo alikuwa hajamhoji mbunge wala dereva wake lakini kapata conclusion hivyo tu.Kashimo kenyewe anatuonyesha kalikosababisha ajali kadogo- si kakuagusha cruiser au hata hilux.
Tatu hata Tanzania Daima sasa inageuka na kudai kwamba ilikuwa uzembe wa dereva wa mbunge- wnadai wamezungumza na dereva wa lori ambae alikwenda ofisini kwao.Jana walikuwa wa gazeti la kwanza kutoa taarifa kwamba kulikuwa na lori ilihusika katika hii ajali- magazeti mengine hayakusema hivyo. Comments kwenye blog hii ndiyo ilikuwa taarifa ya kwanza kabisa kusema kulikuwa na lori iliyokimbia ajabu baada ya ajali. Huyu dereva mbona wa ajabu, imetokea ajali hakusimama, taarifa zinamtaja yeye kugonga gari la mbunge alafu haendi polisi anakwenda kwenye gazeti la Tanzania Daima!!!
Mchoro wa ajali wa Polisi kwa Taarifa hauonyesjhi hata picha ya lori!!!Kana kwamba haikuwepo lori kabisa!!!!
Lori ilikuwa na viyoo tinted na kabla tu ya kuigonga gari ya mbunge dereva wa lori aliteremsha kioo na kuiangalia kwa chini gari ya mbunge ilipokuwa ikimalizia kumpita akaibetua gari ya mbunge pembeni kwa nyuma. Patamu hapa ndugu yangu.Kuna kampeni ya kuficha ukweli wa yaliyomsibu mgombea haki wetu mbunge wa Kyela alipogongwa juzi!!!
Kama jasiri ndugu yangu weka maoni haya na utaona kama hukupatwa na virusi.

1 comment:

Anonymous said...

The good is God is ours! Period... Tuko macho, hatujalala na hatulali.