Friday, June 19, 2009

DECI VUNAVUNA, KILIO



Wakati Deci inadaiwa na wanachama wake zaidi ya Bilioni 20, wananchama na viongozi walioandamana juzi hadi mahakama ya Kisutu kushinikiza viongozi wao waachiwe wamefikishwa mahakamani kwa kosa la kukusanyik ana kusababisha uvunjifu wa amani.



KIKOSI Kazi kilichoongozwa na gavana wa Benki Kuu (BoT), kuichunguza taasisi ya Deci, kimebaini kuwa taasisi hiyo inatakiwa kutafuta njia mbadala kupata zaidi ya Sh20bilioni ili iweze kuwalipa wanachama wake.

Ripoti ya uchunguzi huo iliyosomwa jana bungeni na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustapha Mkulo imeonyesha kuwa, Deci inadaiwa Sh39.272 bilioni wakati akiba yake ni Sh14.4 bilioni tu.

Mkulo alisema wanachama wapatao 343,500 ndio wanaoidai taasisi hiyo.

Mkulo alisema fedha hizo ambazo zilihifadhiwa kienyeji, zitashikiliwa hadi kesi ya msingi dhidi ya viongozi wake itakapotolewa maamuzi mahakamani.

Ripoti hiyo imekuja wakati ambao wanachama wa Deci wamepagawa zaidi, hasa baada ya viongozi wa taasisi hiyo kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuendesha mchezo wa upatu, hali iliyofanya wanachama kuvamia Mahakama ya Kisutu wakishinikiza waachiwe huru.

Waziri Mkulo alisema kikosi kazi hicho kilibaini jumla ya Sh11.828 bilioni zilizokuwa nje ya mfumo wa kibenki.

Kuna wale ambao wamewahi kuvuna mara moja au zaidi na wamepanda tena kwa matarajio ya kuingia katika mzunguko mwingine wa kuvuna, hawa pia watapenda warejeshewe fedha zao, alisema Mkulo.

Kwa maana hiyo, deni la Deci kwa washiriki wake ni kubwa zaidi kuliko inavyoonyeshwa, na uwezo wa kuwalipa washiriki ni chini ya kiasi hicho kilichoonyeshwa.

Hivyo, jinsi na namna ya washiriki wa Deci watakavyorudishiwa fedha zao, ni busara tukasubiri kesi ya viongozi wa Deci iliyoko mahakamani ikamilike.ÓÊÊ

Kuhusu jinsi Deci ilivyokuwa ikihifadhi fedha hizo, Waziri Mkulo alisema pesa hizo zilipatikana majumbani kwa viongozi hao na katika ofisi za matawi mbalimbali, huku nyingine zikiwa zimehifadhiwa katika makabrasha au mifuko.



No comments: