Thursday, June 18, 2009

HIVI CUF WAMEFULIA?

Siku za karibuni chama cha CUF kimeonyesha kupoteza mwelekeo (kama wanavyosema siku hizi wamefulia), inasemekana hakina hata diwani mmoja Tanganyika wachilia mbali Mbunge. Chama hiki kilichosemekana kina nguvu sasa kina kila dalili za kufulia.
Wanafukuzana, wengine wanajiondoa na mengine sijui, labda tusome sehemu ya walaka wa Rwakatare, Naibu Katibu Mkuu aliyejivua uongozi wa chama hicho.


"Na nikanukuu usemi wa kiingereza “wrong diagnosis wrong Treatment” na nikatoa ushauri wa kukutaka Mhe. Mwenyekiti uunde Kamati ya wataalam na wazoefu wa shughuli za kiuchaguzi walio ndani ya chama na hata nje mkae na kutengeneza mfumo, mbinu na utaratibu utakaokiwezesha chama kurejesha ari ya kupendeka na wagombea wetu kuchaguliwa na kushinda chaguzi. Ushauri ulioonekana si muhimu kwa sasa na nikapuuzwa.

Mh Mwenyekiti; naomba sasa nimkabidhi barua yangu ya kujiuzulu Mhe. Katibu Mkuu ambapo uamuzi huu unaanza mara baada ya kumkabidhi barua hii. Najua kujiuzulu kwangu kutapelekea kutolewa tafsiri mbali mbali zilizo za kweli na zisizo za kweli.

Najua kujiuzulu kwangu kutawasononesha na kuwakwaza wengi,
Najua kujiuzulu kwangu kutawafaidisha baadhi ya watu ambao sasa watapumua na kujisemea kama wahaya wasemavyo “TWAMWIYUKAO” AU KWA TAFSIRI “BORA
AONDOKE ALIKUWA AMETUKALIA PABAYA”

Mimi kwangu yote ni mazuri tu; tunapaswa tumuachie Mwenyezi Mungu; “Ni Kheri
Nusu shari kuliko shari kamili”

Nilipokutana na Mhe. Katibu Mkuu kwa maongezi wiki mbili baada ya kupumzishwa Unaibu Katibu Mkuu na kuteuliwa Bw. Joran Bashange; nilimwambia Katibu Mkuu kuwa siku ya Jumapili baada ya Uteuzi nilikwenda kanisani na baada ya Ibada niliamua nimuone mchungaji wangu wa kanisa nimweleze yaliyokuwa yamenielemea moyoni mwangu. Mchungaji baada ya kunisikiliza hakuwa na maneno marefu bali alisema;

“Sikiliza Wilfred; Maandiko matakatifu katika Biblia yanasema, kila jambo linalotokea Duniani na kila linapotokea Mungu ana makusudi katika jambo hilo” Na akazidi kuniambia; “SHUKURUNI MUNGU KWA KILA JAMBO”
Maneno hayo ndiyo yanayonipa nguvu na faraja hadi leo na kesho.

Mhe. Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Mhe.Katibu Mkuu na Waheshimiwa wajumbe wa Baraza Kuu.

NAWASHUKURUNI SANA KWA KUNISIKILIZA"
Wilfred Lwakatare

MCHANGO NA MAONI NILIYOYATOA NDANI YA KIKAO CHA BARAZA KUU LA TAIFA,
CHA TAREHE 09/06/2009
KATIKA AGENDA YA KUTOKANISHA
MUHTASARI WA KIKAO CHA BARAZA KUU CHA TAREHE 28/2/2009.

1 comment:

Nautiakasi said...

Kufukuzana ndio dalili ya kukomaa kichama (hata CCM hufukuzana), kwani ni ishara kwamba wanawanachama wengi wanaoweza kuwa viongozi wa nafasi walizowafukuza wengine.

Pia ni dalili ya kwamba chama hakiendeshwi kwa kujuana, ukivurunda nafasi yako unakwenda na maji tu...!

Kutokuwa na diwani hata mmoja Tanganyika si dalili ya kufulia kwa CUF(kama unavyodai), LAKINI hiyo ni dalili ya uwandawazimu wa WATANGAVYIKA, wanaoendelea kuikumbatia CCM kwa kuhongwa vitenge na kofia na chumvi tu, wakati wa uchaguzi, huku wakibaki kuwa maskini wakutupwa!
Labda nikuulize swali moja; Hivi ukiwa unaendesha gari yako unatoka Dar unaenda morogoro, njiani ukakutana na "chizi" anatembea kuelekea huko huko morogoro, ukaamuwa kumpa lift, lakini akakataa (akahiyari kuendelea kutembea tu), jee aliefulia ni nani??? wewe mwenye usafiri unaetaka kumsadia lakini hataki au yeye anaekataa kusaidiwa???
Basi ukweli ndo huo...watanganyika wamefuliaaaaaaaa! Wazanzibar ni wajanja zaidi, ndo maana hawajaikumbatia CCM inayowafanya maskini kila uchweo kwa malipo ya kanga na chmvi...!
Hakiiiiiiiiiiiiiiiiiiii...!