Friday, June 19, 2009

MIGAGE

Enzi zetu miwa tulikuwa tunamenya kwa meno lakini siku hizi watu lazima wakatiwe vipande vidogo wanalia katika vifuko!!!

5 comments:

Anonymous said...

Hiyo siyo migagi, hiyo ni miwa. Migagi ni mashina ya mahindi yaliyokomaa.

freddy macha said...

Tena kuongezea maneno zaidi ya uliyosema Mzee wa Sumo... Zamani mtu unamaliza miwa hata mitatu huko huko shambani, unajifutafuta tu midomo, unatoka zako, mwepesi, umeshajaza nguvu asilia.
Leo, nyoo.... thubutu!
Tuna meno laini yaliyozoea kula chips na nyama laini. Ukweli maisha yamebadilika.
Lakini ndiyo "maendeleo" hayo. Wengine wanapata ajira (kama huyu mkataji miwa) wengine tunasaidiwa kutafuna...

Anonymous said...

ajabu mzee wa sumo watu siku hizi wanataka wamenyewe na wakati raha ya mua shurti umenyenye kwa meno na utafune mpaka kifundo

John Mwaipopo said...

Kwa kifupi nikiwa Dar es salaam sili muwa kwa sababu kuu mbili. mosi miwa ya dar inatoka mabondeni kunako maji taka ya jiji hili (siyo yote lakini), kwa hiyo najiepusha nayo kwa kuhofia kula 'jnanhii'. na mchicha sili pia.

pili muwa niliouzoea ni ule wa kutoka tukuyu, nauchukua mrefuu naka kivulini, kisha naushughulika mpaka uishe kama alivyosema fredd macha. raha ya muwa uumenye kwa meno yako mwenyewe

Anonymous said...

Mnanikumbusha mbali nyie wote, zama zile tunakwenda shule ya msingi, jioni unakata muwa wako shambani, kesho yake asubuhi unadamka asubuhi kuwa shule umbali kilometa si chini ya tano, unakaribia shule unaangalia uku na uku unakuta hakuna mtu, unaficha muwa wako kichakani. Saa sita na nusu wakati wa kwenda kula unakwenda unachukua muwa wako unakaa na kuula na baadhi ya marafiki, mnajipanguza midomo na kuanza masomo ya mchana