Friday, June 19, 2009

THE UTAMU

BREAKING NEWS

Polisi wa Tanzania kwa kushirikiana na Polisi wa Kimataifa

(Interpol),wamefani kiwa kumshika Raia mmoja wa Uingereza ambaye ana

asili ya Tanzania Ndg Malecela Peter Lusinde (pichani) mwenye umri wa

miaka 39 na kutuhumiwa kwa kuundesha mtandao wa Ze Utamu. Ndugu

Malecela ambaye anajulikana pia kwa jina la "Male" ni Mtaalamu wa

kompyuta na ana uwezo wa kuzungumza na kuandika Kiingereza,kiswahil na kichina ana makazi katika mji wa Essex nchini Uingereza.

Wataalamu wa Idara ya upelelezi kutoka Tanzania wakishirikiana na

wenzao wa Uingereza wamefanikiwa kuonana na Ndg Male na kupata

ushahidi wa kutosha kwamba ndiye alikuwa mmiliki wa Mtandao huo.Idara

ya Upelelezi na polisi wa Uingereza wameutaarifu Ubalozi wa Tanzania

mjini London kuhusu suala hilo.Maofisa Ubalozi Mr.Clement Kiondo na

Amos Msanjila wamefahamishwa jambo hilo.Malecela ni Mtoto wa Mzee Job

Lusinde ambaye amewahi kufanya kazi kwenye nyadhifa mbalimbali za

utumishi wa serikali Nchini Tanzania.

Habari zilizothibitishwa zinadai kuwa Ndg Malecela amerudishwa

Tanzania kwenda kujibu tuhuma mbalimbali za kuendesha mtandao uliokuwa

unadhalilisha watu,kuna malalamiko 6850 yaliyoandikishwa kulaumu

udhalilishwaji wa watu uliofanywa na mtandao huo,Mtandao huo

ulisimamishwa mwanzoni mwa mwezi wa pili kwa maombi ya serikali ya

Tanzania baada ya kutoa picha ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya

Muungano Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete,ufuatiliaji uliofanywa baada ya

picha hiyo ndio umepelekea kukamatwa kwa Ndg Malecela.

Haijaeleweka wazi Ndg Malecela atashitakiwa kwa sheria gani? Lakini ni

wazi kwamba atashitakiwa Nchini Tanzania. Licha ya Ndg. Malecela

Polisi wa Upelelezi wamezungumza na Watanzania wengine wawili katika

miji ya Wichita na San Diego Nchini Marekani, ambao pia wanahusishwa

na Mtandao huo wa Ze Utamu.


Habari hii imefika ghafla kutoka rsmiruko.blogspot.com samahani uthibitisho utakuja baadae, nasafiri kidogo!!

No comments: