Wednesday, July 15, 2009

YA NGELEJA

Bwana waziri alifika Ubungo kuzindua mtambo wa kusindika gesi kwenye mitungi kwajili ya matumizi ya nyumbani na kwenye magari. Kwa nia njema tu!!
Ghafla wananchi wakaibuka na kuanza kulalamikia haki yao ya fidia ili waondoke eneo hilo, jamaa walivamia kiasi cha kumfanya waziri kuacha shuguli iliyomleta ili awasikilize!
Akajieleza kisawasawa ili kuwapooza watu hao lakini wapi!!
Akafafanua weee mpaka kijashio kikamtoka, kweli wabongo wamebadilika, wanadai haki zao kwa nguvu kubwa sasa sijui Shukuru Kawambwa akienda kwa wakazi wa Kipawa wanaodai fidia ili kupisha uwanja wa ndege kwa zaidi ya muongommoja itakuwaje?

No comments: