Thursday, August 20, 2009

UTUMBO SOKONI

Angalau sasa hivi wauza utumbo wameanza kuweka mazingira masafi kidogo kwa ajili ya tunaopenda kitoweo hiki. Kinakuwaga kitamu lakini ukikutana na inzi wakikizunguka ngumu kununua!! Hivi Ng'ambo kinauzwa?

7 comments:

Anonymous said...

Bro, kinauzwa ughaibuni, nimekiona mabuchani Finland, Sweden, France na Belgium. Lakini sijaona Watanzania wengi kukinunua. Wanunuzi wakuu wa kitoweo hiki ughaibuni ni Wakongo na Wanaijeria.

Anonymous said...

ndiyo kinauzwa hapa USA lakini ninasafishwa mno mpaka radha inakimbia pia

Anonymous said...

mimi sijaona mitaa ya hapa USA

Anonymous said...

nenda Fiesta kama uko DFW area

Anonymous said...

na kama ukitaka harisi kabisa kama Bongo nenda machinjioni ya hapa DFw area

Anonymous said...

Hapa UK nimekiona pia,lakini kama alivyosema mdau hapo juu,wanakisafisha mno mpaka radha inaondoka.Hicho raha yake kiwe na ule uchafu,kiwe kimeoshwa fasta kwenye mto msimbazi,hapo ndo kinakua kitamu.

John Mwaipopo said...

ukisikia kupanuana mawazo kwa blogu ndio huku. nimeipenda sana hii post na comments zake