Tuesday, February 23, 2010

MANOARI


Manowari ya Kivita ya Marekani iitwayo USS Farragut ambayo ilizuia shambulizi la kiharamia lililofanywa dhidi ya Meli ya Kitanzania MV Barakaale 1 hapo Februari 21, na kuwakamata maharamia waliohusika katika tukio hilo. Baada ya kupokea taarifa ya kuomba msaada kutoka kwa Nahodha wa MV Barakaale, Helikopta aina ya SH-60B Seahawk kutoka katika Manowari ya Jeshi la Marekani iitwayo USS Farragut iliwasili na kuzuia mashambulizi mawili dhidi ya meli hiyo ya Tanzania.

Manowari Farragut ni sehemu ya kikosi maalumu cha kimataifa kijulikanacho kama Combined Task Force 151, kilichoundwa Januari 2009 kwa lengo la kuzuia, na kupambana na uharamia ili kulinda usalama wa vyombo vya usafirishaji majini na kuhakikisha kuwa vyombo hivyo vinakuwa na uhuru wa kupita katika eneo hilo kwa faida ya nchi zote.

1 comment:

mwanakijiji said...

Mkuu.. hiyo ni Merikebu na siyo Manowari.. manowari ni submarine au wakati mwingine wanaita nyambizi, hivyo inaweza kuitwa "meli" au meli/rikebu.. shukrani.