Monday, February 22, 2010

MAONYESHO YA MAGARI

Inspekta wa polisi akiwa amemweka chini ya Ulinzi Paul baada ya kuzungusha gari pale Mlimani City.
Watanganyika wenzake wakakomaa aachiwe kwa kuwa waliridhika na shoo yake!
Wakaongezeka na kukomaa zaidi ili gari liondoke bila kutiwa nguvuni!
Paul akifanya mambo na gari lake Toyota Celica am,balo enzi hizo lilifanya kweli katika mashindano ya Safari Rally!
Bingwa wa Afrika Jamie Whyte akifanya mambo katika viwanja vya mlimani City!
Mashabiki wakishuhudia umahili wa madereva!
Kila kona ilijaa mashabiki!
Polisi ilibidi kudhibiti wananchi ili kuweka usalama na kutahadharisha maisha ya watu yasidhuliwe!
Sikutegemea kwamba Dar es Salaam ina washabiki wa kutosha wa mbio za magari na hii ilijidhihirisha mwishoni mwa wiki wakati madereva wanashindana katika Michuano ya kimataifa walipoonyesha uwezo mbele ya halaiki ya watu.
kali ilitokea wakati Mbongo mmoja anayeitwa Paul alipoingia na gari lake Celica na kuipiga riound kali kuliko hata madareva weliokuwa katika utaratibu na kufanya polisi kutaka kumkamata, lakini wananchi walipiga kelele aachiwe na nguvu za umma zikashinda.
Lakini baadae du mtanganyika huyo akajikuta lupango eti kwa kuvuruga mashindano!!!
wengine wanadai huwa ana hamu ya kushiriki lakini hukataliwa kupewa namba kutokana na gari lake, sasa michezo kama hii itabakia mpaka lini kuwa ya wahindi na wazungu tu!!!!!!!

No comments: