Thursday, March 25, 2010

MBEYA

Msimamizi mkuu wa kazi waka kampuni ya ujenzi wa uwanja ndege wa Songwe ya Kundan Singh Consruction limited Mhandisi Nderitu Peter akitoa maelekezio juu ya maendeleo ya ujenzi huo.

UJENZI wa Uwanja Mpya wa ndege wa Songwe Mkoani Mbeya, unatarajia kukamilika mwezi Oktoba Mwaka huu 2010 baada ya kukamilisha ujenzi wa hatau mbili za Mwisho zilizobaki.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Viwanja vya Ndege Tanzania Mhandisi Prosper Tesha mradi wa ujenzi wa uwanja huo ulianza mwaka 2001 ukiwa umesanifiwa kwa matumizi ya ndege ya ukubwa wa wastani wa abiria 50 (sawa na ndege forker 50) na ulipangwa kukamilika mwaka 2005.
Tesha alisema kuwa wakati mradi unaendelea Serikali iliamua kuupanua mradi na kufanya usanifu upya wa Kiwanja na kuweza kuhudumia ndege kubwa zenye kuweza kubeba wastani wa abiria 100 (sawa na Boeing 737).
“Iliamuliwa pia mradi utekelezwe kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha kwa hiyo awamu ya kwanza ilianza mwaka 2001 na kukamilika 2004,ya pili iliana 2004 na kukamilika 2007 na awamu ya tatu ndiyo inayoendelea ilianza mwaka 2008 inatazamiwa kuikamilika 2010.”alisema
Alisema kuwa katika utekelezaji wa awamu ya tatu mradi ulitakiwa kumalizika katika miezi 18 yaani mwezi April 2010 na kwamba hadi kufikia sasa mradi umetekelezwa asimilia 25 pekee wakati kimkataba mradi ulitakiwa kuwa umekamilika kwa asilimia 90.
Kwa upande wake msimamizi mkuu wa kazi wa kampuni inayojenga uwanja huo ya Kundan Singh Consruction limited mhandisi Nderitu Peter alisema kuwa bado hatua mbili za ujenzi ili kuweza kamilika kwa uwanja huo.
Alisema kuwa uwanja huo una urefu wa kilometa 3.33 na upana wa mita 45 na kwamba hali iliyofikia kwa sasa ya ujenzi wa uwanja ndege yoyote inayostahili kutua inaweza kutua kama itapata idhini kutoka mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania.

1 comment:

Ava said...

An amazing read! Thanks :)
Ava

exercises to lose belly fat