Monday, March 08, 2010

KIFO CHA MAALIM SEIF
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad akionekana katika picha tofauti leo akiwa amepumzika kwenye hospitali ya Shree Hindu Mandal ya jijini Dar es Salaam. "Sijafa" yalikuwa maneno ya awali kabisa maalim Seif alipowaona waandishi habri waliofika kumjulia hali kwenye wodi aliyolazwa hospitalini hapo.
Akiwa na walinzi wake, Maalim Seif alitabasamu na kuongeza kuwa alipelekwa hospitalini hapo baada ya msukumo wa damu kupanda ghafla (Blood Pressure) na kuamuliwa akimbizwe hospitalini Ijumaa jioni ya Machi 5, 2010. "Najisikia mzima kabisa na ninachosubiri ni ruhusa tu ya daktariwangu" alisema Seiff maarufu kama Maalim Seiff. (Habari Picha na Khalfan Said

No comments: