Monday, July 12, 2010

MABOMU KAMPALA

Milipuko miwili iliyotokea jijini Kampala imeua watu wanaokadiriwa kuzidi 64, mmoja wao akiwa mmarekani wakati wakiangalia fainali za kombe la dunia.
Mlipuko mkubwa ulitokea katika Club ya Rugby ambako watu wengi waliokuwa wakiangalia fainali ya Hispania na Holland walikufa wakati katika mgahawa wa kiethiopia wamerekani watatu walijeruhiwa. Watu 49 wamekufa katika Club tya Rugby na 15 katika mgahawa.Polisi wa Kampala wanaamini milipuko hiyo imefanywa na kundi la waislamu wenye siasa kali la Al Shabab la Somalia na kuwas lina uhusiano na Al Qaeda.“Nakumbuka kupoteza fahamu baadae nasikia watu wakikimbia na kupiga mayowe” anaelezea Klis Sledge ambaye ameumia mguu na kuungua uso akiwa hospitali. “Napapenda hapa lakini sijui kwa nini hii imetokea..na sijui nani kafanya hivyo”.

No comments: