Wednesday, July 14, 2010

MWAIKUSA AKINDILE

Mhadhiri mshiriki wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Profesa Jwani Mwaikusa, mpwawe na jira wameuawa na majambazi usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake.

Sambamba na mauaji ya Profesa Mwaikusa, majambazi hayo pia yaliua mtoto aliyekuwamo ndani ya nyumba ya Profesa huyo, Gwamaka Daudi na jirani John Mtui.

Polisi wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa jirani huyo ambaye alikuwa na bastola aliuawa alipokuwa akienda kutoa msaada kwa Profesa huyo.

Jumuia ya wafanyakazi na anafunzi wa UDSM walikumbwa na simanzi kuu leo baada ya kupokea taarifa hizo ingawa wanafunzi walikuwa wakiendelea na mitihani ya kumaliza mwaka.

Mkuu wa Kitengo cha Sheria Chuoni hapo Profesa Palamagamba Kabudi, alisema kifo cha Profesa Mwaikusa siyo tuu pigo kwa chuo hicho bali tasinia nzima ya sheria na taifa kwa ujumla.

Kwa mujibu wa Profesa Kabudi, mpaka wakati kifo kinamkuta Profesa Mwaikusa alikuwa, Profesa Mshiriki katika idara ya Sheria za Umma (public law).

Alisema Profesa Mwaikusa alizaliwa Julai 21 mwaka 1952, na kuwa aliajiriwa kama mhadhiri msaidizi na chuo hicho mwaka 1986. Alisomea sekondari ya Mirambo, Tabora.

No comments: