Tuesday, July 13, 2010

KITI CHA IKULU

Kuna kitu kilikuwa kinanisumbua kwa muda mrefu tokea wakati wa utawala was Rais Mkapa.
baada yakuumia mguu baadae wasaidizi wake walikuwa wanazunguka na moja ya viti vilivyopo Ikulu ili aweze kukalia katika hafla mbalimbali nchini na mara nyingine nje ya nchi.
Lakini baada baada ya Kikwete kuingia madarakani hicho kiti kimekuwa kikiwekwa kila sehemu hadi mikoani anaposafiri!
sasa ninachojiuliza kile ni kiti cha Rais ama cha Ikulu, maana mi nilidhani ilikuwa kinamsaidia Mzee Mkapa wakati mguu unamuuma!
Labda kuna wengine mnajua utaratibu wa viti hivyo. Nawasilisha.
Hapa kiti hicho nyuma ya Rais wakati mama maria Nyerere alipomtembelea Ikulu hivi karibuni.

No comments: