Monday, July 12, 2010

UCHAGUZI 2010

MKUTANO mkuu wa chama cha wananchi cuf wilaya ya Morogoro mjini umemchagua Hajira Silya kuwa mgombea ubunge viti maalum kwa tiketi ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Hajira Silya ambaye ni mwanachama wa siku nyingi wa chama hicho ameibuka na ushindi huo baada ya kupata jumla ya kura 112 dhidi ya kura 98 alizopata mpinzani wake katika nafasi hiyo bi.Vennie Mlangwa.
Wakati Silya akiibuka na ushindi huo katika viti maalum,mwenyekiti wa zamani wa chama hicho wilaya ya Morogoro mjini Abeid Mlapakolo yeye amechaguliwa kuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho katika jimbo la Morogoro mjini.
Mlapakolo amefanikiwa kupata nafasi hiyo baada ya kupata jumla ya kura 136 za ndiyo kati ya kura 204 zilizopigwa akiwa mgombea pekee katika nafasi hiyo baada ya Mbalala Mahragande aliyetangaza kuwania nafasi hiyo hapo awali kujitoa.

2 comments:

Anonymous said...

kila la kheri mama yetu mpendwa sisi tupo pamoja na wewe kwenye nia pana njia utafika tu

Anonymous said...

honera sana mama ye2 kwa kuchagulia ingawa tupo mbali nawe watanzania waishio huku sweden wanakupongeza sana kila la kheri mama.sameed jameel sanura sigwa and my wife 2 be evelina lundström tunakupongeza sanaaaaaaaaa