Tuesday, July 13, 2010

YANGA TABATA


Wagombea nafasi mbalimbali za uongozi katika Klabu ya Yanga kesho saa moja jioni watakutana na wanachama ili kujinadi katika tawi la Tabata Shule.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa Tawi la Yanga, Kimanga, Pastory Kyombya alismea wagombnea wane wameomba kukutana na wanachama katika mkutano utakaoanza saa 1.00 jioni katika ofisi za tawi hilo.
“Ni wagombea wane tu ambaio wameppangiwa kukutana na wanachama wa matawi ya Tabata, Kimanga, Uwanja wa Twiga, Segerea na Kinyerezi . Hivyo kama kutakuwa na wengine tutawapa nafasi ya kukutana nasi” alisema Kyombya.
Kyombya aliwataja wagombea watakaopata nafasi ya kujinadi kwa wanachama hao kuwa ni Mgombea urais, Francis Kifukwe, Makamu, Denuis Mosha na Jackson Maagi na Lameck Nyabaya ambao wanagombea ujumbe kutoka tawi la tabata Shule.
Mwenyekiti huyo aliwataka wanachama wa Yanga kutoka katika matawi hayo na mengine ya jirani kujitokeza kwa wingi ili waweze kujua wagombea hao wataeleza nini juu ya kuendeleza klab hiyo kongwe baada ya kuingia madarakani.

No comments: