Friday, September 03, 2010

MSIBA MZITO BUKOBA

Baba mzazi wa Reginald Miruko (Kisima cha Fikra) Mzee Simon Miruko amefariki dunia jana mchana. Leo asubuhi Reggie ameanza safari ndefu ya kwenda Kaskazini Magharibi mwa nchi (Bukoba) kwa ajili ya kumpumzisha baba yake.
Mzee Miruko (84) maarufu kama 'Tasimon' alifariki baada yakuugua kwa muda na anatarajiwa kuzikwa kwao Kamachumu baada ya watoto wake kuwasiri.

MUNGU AMREHEMU NA KUWAPA NGUVU WANAFAMILIA, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI KATIKA KIPINDI HIKI CHA MSIIBA

“Ndg yetu Reginald, kifo ni udhihirisho wa Umungu. Kwamba hakuna kilichopo duniani isipokuwa kwa uweza wake Mwenyezi. Baba amelala katika usingizi ambao sote twatarajia tutaamka naye pale parapanda itakapopigwa. Kwa hiyo yeye ametangulia, sisi tutamfuata. Tunamkosa kwa muda mfupi sana. Kibinadamu itatupasa kusononeka. Ndio maana nakupeni pole sana wanabidii na hasa Reginald na jamaa yako yote. Mwenyezi ampumzishe mwanae, baba yetu katika amani-AMINA.” –MASHAKA MGETA

No comments: