Monday, September 06, 2010

SLAA NA MAMA SLAA

Dk Slaa anamtambulisha mgombea ubunge wa Hanang na aliyekuwa mkewe, Rose Kamili, katika eneo la Endosak, jirani na nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye

IKIWA leo ni siku 14 tangu kampeni za uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani zilipozinduliwa Agosti 21, hali ya kampeni imegeuka kuwa vita ya kuchafuana kinyume na matarajio ya wengi.

Mbali ya kuchafuana kiasi kwamba imani kwa wananchi inaanza kupungua, baadhi ya wagombea wa nafasi za wabunge wameibuka na madai mazito yakiwemo ya kudaiwa kutaka kuuawa kwenye majimbo yao.

Kampeni za kuchafuana zinazoonekana zaidi kuelekezwa kwa mgombea wa urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, kuhusiana na suala lake la ndoa.

Hali hiyo, inatafsiriwa na wachunguzi wa masuala ya siasa kuwa ni mchezo mchafu uliondaliwa na wapinzani wake kumchafua mbele ya jamii ili aonekana haifai.

Hivi sasa, vigogo kadhaa wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wanadaiwa kununua baadhi ya magezeti na kuyasambaza katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro huku yakiwa yamepambwa na habari kuhusiana na maisha ya ndoa ya mwanasiasa huyo.

Hali hiyo, imedhihirika mwishoni mwa wiki, baada ya gazeti moja linalotolewa kila wiki, kugawiwa bure kwenye mikoa hiyo na wauzaji wa magazeti waliodai kupewa maelekezo maalum na vigogo wa CCM.

Jambo jingine, linaloonekana sasa ni rufaa nyingi zilizowasilishwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kuhusiana na pingamizi zilizowekwa na wagombea wa vyama vya upinzani.

Vyama vya upinzani, vimekuwa vikilalamimika kuchezewa rafu na wagombea kadhaa wa CCM wakiwemo mawaziri ambao wanadaiwa kutumia nyadhifa kuwakandamiza wapinzani wao.


No comments: