Tuesday, October 26, 2010

SHIBUDA HURU

Mgombea wa Chadema jimbo la Maswa John Shibuda,kaaachiwa huru na polisi kwa maelezo kuwa hakuhusika kwenye mauaji ya dereva wa gari la CCM, huku kamati ya maadili ya uchaguzi ya wilaya ikiandika barua kutaka kada huyo wa zamani wa chama tawala aenguliwe kugombea.

Wakati hayo yakiendelea, Jeshi la Polisi limesema linaendelea kuchunguza tuhuma za mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM, Robert Kisena kumshambulia na kumbwaga chini kamanda wa polisi wa wilaya, ikisema iwapo atabainika kuwa alihusika atafikishwa mahakamani.

Watu wengine 11 wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa Chadema jana walifikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuhusika kwenye vurugu dhidi ya wafuasi wa CCM zilizosababisha mtu mmoja kupoteza maisha.

Shibuda na Kisena walikamatwa na polisi baada ya kutokea vurugu kubwa baina ya wafuasi wa Chadema na wa CCM karibu na eneo ambalo chama hicho cha upinzani kilikuwa kikiendesha mkutano wake wa kampeni za ubunge na vurugu zilisababisha dereva wa mgombea huyo wa CCM, Steven Kwilasa kupoteza maisha.

Wakati Shibuda alifuatwa na polisi kwenye mkutano huo wa kampeni Oktoba 21 na kuwekwa ndani tangu siku hiyo akituhumiwa kuhusika kwenye vurugu zilizotokea takriba kilomita moja kutoka sehemu alipokuwa, Kisema alikamatwa Jumapili akituhumiwa kumshambulia kamanda huyo kwa mateke akiwa kituo cha polisi. Alihojiwa kwa saa kadhaa kabla ya kuachiwa huru.


Afisa mkuu wa upelelezi wa Mkoa wa Shinyanga, Seleman Nyakipande ambaye pia ni mjumbe wa tume iliyoundwa kuchunguza vurugu hizo inayoongozwa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Robert Manumba, aliiambia Mwananchi kuwa Shibuda ameachiwa kwa dhamana jana jioni.


Alisema kuwa Shibuda alikidhi masharti yote ya dhamana aliyowekewa na kwamba kwa sasa yupo huru na kuongeza kuwa moja ya masharti aliyopewa ni kupatikana wakati atakapohitajika na jeshi hilo.

Mtanange umerejea palepale siku tano tu zimebaki kw ampiganaji huyu ili arejee bungeni na tiketi nyingine!

No comments: