Friday, December 10, 2010

KUMBUKUMBU

Leo ni miaka mitatu tokea kufariki kwa Baba yetu Mpendwa Daniel Bukuku nyumbani kwake, Msalato Dodoma. Unakumbukwa sana na Mama, Alice ambaye kwa sasa amebaki mpweke, watoto wako Ambata, Francis, Gwamaka Nsubi, Mpoki Neema na Naomi na wakwe zako Shameem, Neema, Joyce, Lilian, George na David, wajukuu wote, ingawa wameongezeka kwa sasa.

Tunashukuru kila mmoja kwa kutuwezesha kumlaza salama wakati huo na kwa maombi katika kipindi chote.

Daima tutakumbuka ukaribu wako, 'upole' na ucheshi wako

Tunaamini kuwa tutaonana siku moja Paradiso. Amen

No comments: