Wednesday, December 29, 2010

MAANDAMANO YA CUF JANA

polisi walibeba vya moto!!
Jamaa wakaingia ndani na kukabidhi rasimu yakatiba.
Baadae Itatilo akatoa taarifa ya kupokelewa wizarani.
Baadae akaonyeshwea TZR ya kuingia kwenda kunako sheria za kipolisi jamii.
LAkini wananchi walifanikiwa kuandamana.
wakasema la moyoni.Haikujalisha umri.
Vijana walionyesha wazi wanachokitaka.
Baadae ilikuwa kusherehekea ushindi tu!
CHAMA Cha Wananchi (CUF) jana kiliwazidi ujanja polisi waliokuwa wakidhibiti maandamano yao baada ya kufanikiwa kuyafanya na kuwasilisha rasimu yao sifuri ya katiba kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria. Polisi hao walikuwa wanazuia maandamano hayo kutekeleza agizo la Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Suleiman Kova aliyolitoa juzi kuzuia maandamano hayo kwa kile alichoeleza kuwa ni batili.

Katika maandamano hayo yaliyosimamisha kwa muda shughuli za kiuchumi na kijamii, wafuasi na wapenzi wa chama hicho wakiongozwa na Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro, walifanikiwa kuingia barabarani na kuwasilisha rasimu yao ya katiba kama walivyopanga. Hata hivyo maandamano hayo yaliyoanzia Buguruni Sheli hayakuanza saa 2:00 asubuhi kama yalivyopangwa kutokana na mvutano ulioibuka baina ya waandamanaji hao na polisi wenye silaha ambao walifika ofisini hapo kuwadhibiti.

No comments: