Monday, December 13, 2010

NGUMI WAPIGWA JEKI

Faraji Sayuni akipokea masumbwi kutoka kwa Ramadhani Kumbele.
Hamis Ajali akimtwanga Novert Damian.
Mtoto Zahor Shauri (13)akimtandika sumbwi la uso Omary Ramadhani (14)wakati wa pambano la utangulizi katika hafla ya kukabidhiwa kwa ulingo wa masumbwi uliotolewa na Mkurugenzi wa kampuni ya Bold Air, John Ndugulu Shirikisho la Masumbi nchini (PST) na kuzinduliwa na Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi, Keko jijini Dar es Salaam

Rais wa Shirikisho la Masumbwi Nchini (PST), Emamanuel Mlundwa akimwonyesha Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi uliongo wa masumbwi masumbwi uliotolewa na Mkurugenzi wa kampuni ya Bold Air, John Nduguru (Kushoto) kabnla ya kuuzindua jana







Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na michezo Emmanuel Nchimbi amewataka watanzania kujitolea vifaa vya michezo ili kusaidia kuinua vipaji vya vijana nchini.





Akizungumza jijini Dafr es salaam alipozindua ulingo wa ndondi aulitolewa na Mkurugenzi wa kampuini ya Bold Air, John Ndungulu, Waziri Nchimbi alisema yuko tayari kushirikiana na kusaidia watu wanaojitolea kwa ajili ya kuendeleza michezo.





“Nimefurahi sana kuona ulingo ni mzuri na unafaa kwa ajili ya kuandaa vijana wetu, naomba usiishie hapa tu bali waeleze watanzania wengine waishio marekani na nchi nyingine wajitokeze kusaidia michezo” alisema.





Nchimbi ambaye alishuhudia mapambano ya ndoni ya watoto na vijana katika viwanja vya Keko Mambembea alisema wizara yake inaweka mikakati ya kuitangaza nchi kwa kupitia michezo.





Mwenyekiti wa Shirikisho la Masumbwi laTanzania (PST), Emmanuel Mlundwa alisema kuwa kupatikana kwa ulingo huo utasaidia si tu ngumi za kuilipwa bali hata za ridhaa kwani ulingo uliokuwepo ulinunuliwa miaka ya sabini.





Alisema pamioja na kutokuwepo kwa ulingo bora kwa kipindi chote lakini watanzania wameweza kufanya vyema na kuwepo kwa mabingwa wadunia katika ngumi za kulipwa na kick boxing.





Nae Mkurugenzi wa Bold Air, Ndungulu aklisema kuwa amejitolea ulingo huo ukiwa ni mwanzo tu katika kusaidia michezo nchini na yuko tayari kusaidia nyanja nyinge za michezo ikiwemo ngumi.





“Tanzania hatujuklikani sana kama wenzetu Kenya kwa sababu katika michezo tuko nyuma, hata kule Marekani wanachangaa ukiwaambai mtanzania kwa kuwa wanawajua wakenya kutokana na Marathon” alisema na kuongez akuwa kama watanzania wakijitolea katika michezo nchi itanufaika kiuchumi.

No comments: