Monday, December 13, 2010

DOKTA REMMY AAGA!!!


Mwanamuziki wa Siku nyingo Remmy Ongala (Dr Remmy) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Remmy ambaye amekuwa mgonjwa kwa muda mrefu amefia nyumbani kwake Mbezi jijini Dar es salaam.

Ongala ambaye ni maarufu kwa nyimbo zake kama ‘Siku ya Kufa’ na ‘Kifo’ ni mmtanzania mwenye asili ya Kongo ambaye pamoja na kuingia nchini miaka ya sabini ilimchukua muda mrefu kupata uraia wa Bongo.

Wimbo wake wa 'Mbele kwa Mbele' na 'Mambo yote kwa soksi' ndizo zilihitimisha uimbaji wake wa nyimbo za kidunia kabla ya kumpokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wake na kuimba injili.

Mwenyezi Mungu ampe pumziko la milele, awatie nguvu wafiwea wote!


No comments: